Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY YAWANOA MAAFISA KUTOKA SERIKALINI NA SEKTA BINAFSI

Baadhi ya washiriki kutoka The Open University of Tanzania wakiongozwa na Dr. Celia Muyinga wa kwanza kulia- wakiwa na vyeti vyao

Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni Ndugu Lucas Jackson
---------
Katika kuendeleza wajibu wake wa kutoa mafunzo ya muda mfupi, ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY iimeendesha mafunzo ya juma moja ya Itifaki na Uhusiano wa Kibiashara ‘PROTOCOL AND BUSINESS ETIQUETTE SHORTCOURSE kati ya tarehe 22 -25 February, 2017. Mafunzo haya yalilenga kuwaongezea uwezo maafisa mbali mbali kutoka serekalini na sekta binafsi. Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo  ya muda mfupi yatolewayo na ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY  kila mwezi,

katika mafunzo hayo ambayo Kwa kawaida wawezeshaji wa mafunzo hayo ya muda mfupi katika, huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea katika mambo ya Diplomasia na hivyo kuwapa washiriki uzoefu na mafunzo ya kiutendaji zaidi ili kuwajengea uwezo na ufanisi katika kuboresha majukumu yao.


Mafunzo hayo ya wiki moja yaliyofanyika Dar es salaam (katika ukumbi wa mikutano wa Dar es Salaam Convention Centre - DCC), washiriki walijifunza jinsi ya kuratibu itifaki za dhifa, sherehe za kitaifa na mikutano mingine mbali mbali pamoja na kuandaa mikutano ya kibiashara, tabia njema za kibiashara, kanuni za Mavazi na kupokea wageni mashuhuri na kuwahudumia. Pia walijifunza Diplomasia, uhuisiano wa umma na namna bora ya kuandaa taarifa kwa ajili ya mawasiliano na umma, yalihusisha maofisa 24 wa kada mbalimbali kutoka idara za Serikali , vyuo vikuu na sekta binafsi pamoja na maafisa kutoka katika Balozi zinazowakilisha nchi zao Tazania.

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni wa ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY Ndugu Lucas Jackson alisisitiza kwamba mafunzo hayo yatawasaidia maofisa hao kuboresha utendaji wa kazi zao na kuleta ufanisi mahala pa kazi hivyo kuna haja ya waajiri kuwaruhusu wafanyakazi wao kupata mafunzo kama haya na mengine yatolewayo na EONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY ili kuwajengea uwezo watanzania hasa katika Diplomasia ya Uchumi na uchumi wa viwanda Tanzania, na hivyo kuzalisha wataalam wenye weredi wa uchumi wa viwanda na Diplomasia ya Uchumi.

Akizumgumzia mafunzo yaliyohitimishwa ya Protocol and Business Etiquette; alisema
“Kazi zinazohusiana na itifaki na uhusiano wa kibiashara (Protocol and Business Etiquette) zinahitaji utaalam ambao utamfanya mtu aweze kutimiza majukumu yake kwa ufasaha na kufikia malengo na matokeo mazuri. Hivyo mafunzo haya ya kivitendo ya Itifaki na mengine yote yanayotolewa na ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY yana lengo la kuwajengea uwezo na utaalam washiriki wote ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupata matokeo bora,”

Mkurugenzi wa Mafunzo na Operesheni Ndugu Lucas Jackson, akaongeza kuwa, kutokana na uhitaji ECONOMIC DIPLOMACY TRAINING ACADEMY itaendesha  mafunzo ya wiki moja ya UTATUZI WA MIGOGORO NA USULUHISHI (CONFLICT RESOLUTION) mnamo tarehe 22 -25 March 2017 yatakayofuatiwa naya DIPLOMASIA YA UCHUMI ; Biashara na uwekezaji (ECONOMIC DIPLOMACY: Trade and Investment Promotion) mnamo tarehe 5  8April, 2017 hapa DCC Dar es salaam, na kuwataka wale wote wanaohitaji  kupiga namba 0713667303 au lucassoona@yahoo.com kwa maelezo zaidi na kupewa utaratibu.

AU kuwasiliana moja kwa moja na:
Kurugenzi ya Mafunzo na Operesheni,
Economic diplomacy Training Academy
info@economicdiplomacy.ac.tz
Mob: 0763657587
Website: www.economicdiplomacy.ac.tz/training
www.economicdiplomacy.ac.tz
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top