Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JPM 'awatolea uvivu' Makatibu CCM

Dodoma. Mwenyekiti wa Taifa CCM, Rais John Magufuli amewataka
makatibu wa mikoa wa chama hicho wanaotaka kuingia katika vikao vya
Halmashauri Kuu  (Nec) ya Taifa ya chama hicho wakagombee uenyekiti.

Akizungumza leo (Jumamosi) wakati wa ufunguzi wa kikao cha Nec, Rais Magufuli amesema
kuna watu wanaumuhimu wa kuingia katika vikao vya Halmashauri Kuu na
kwamba wakikosa kutakosekana uwakilishi .

“Nikawaambia mbona mwaka uliopita waliposimama wakimpinga mwenyekiti
makatibu mlikuwepo? Wakati mwenyekiti anawalipa mshahara mbona
hamkumtetea? Mbona hamkusimama kupigana na bado wakaendelea  kuimba
wanaimani na mtu fulani na wengine mkawa mnaitikia,”amesema.

Amesema kwa kuwa mabadiliko ya Katiba na Kanuni ambayo yatapunguza
idadi ya wajumbe wa vikao vya juu vya chama hicho walishayajadili
katika  kikao kilichofanyika Desemba 13 mwaka jana, ni matumaini yake
kuwa kikao hicho hakitachukua muda mrefu kuyajadili.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top