Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika ziara ya kukagua sehemu zilizokumbwa na mafuriko katika bonde la Mto Msimbazi, baada ya mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewatahadharisha wakazi wa bonde la mto msimbazi kuwa mvua zinazo nyesha zitaweza kuendelea kuleta madhara kwa wakazi waishio mabondeni kutokana na uharibifu wa miundombinu ya maji.
Makonda amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa bonde la mto Msimbazi ambao walikusanyika kumsikiliza wakati alipokuwa akitembelea maeneo hayo.
"kulingana na utabiri wa hali ya hewa mvua hizi zipo kati ya Milimita 30 hadi 35 na zikiendelea kuongezeka mpaka Milimita 50, maana yake hali itakuwa ni mbaya zaidi hivyo waswahili husema kinga ni bora kuliko tiba "Amesema Makonda
amesema kuwa wao kama Serikali chini ya Rais Magufuli wanategemea kupata fedha kutoka benki ya Dunia ili kuweza kudhibiti na kutengeza mto msimbazi ili kupunguza Madhara, kwani yanayo onekana leo ni tabia mbaya za kwetu wenyewe wanadamu kuwa wakaidi pindi tunapoambiwa tusijenge mabondeni tunakuwa wabishi, pia tunaambiwa tuhakikishe kuwa hatuharibu zile kingo za maji sisi tunaharibu na kuziba kisha kujenga.
Post a Comment