Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Tanzania ya Rais Magufuli inavyosonga mbele



Rais Magufuli aliwahi kusema anataka kuona nchi inakwenda, na kweli nchi inakwenda mbele na hakuna aliyethubutu kujitokeza kumkwamisha.

Tunaona miundombinu (barabara, flyovers, madaraja) yakijengwa kila kona ya nchi. Tunaona idara za mawasiliano na uchukuzi zikiimarika kwa ndege 2 mpya kununuliwa (ndege 3 nyingine mpya zikiagizwa tena), treni na mabehewa yakinunuliwa na kuendelea kufanya kazi, shirika la simu la TTCL likifufuka baada ya Serikali kulimiliki kwa asilimia 100. Hakika nchi inasonga.

Tunaona nidhamu, uwajibikaji na uchapakazi kwa watumishi wa umma vikiimarika sana tofauti na awali. Matendo ya rushwa, ubadhilifu, ufisadi vikipungua sana kipindi cha utawala wa Rais Magufuli.

Tunashuhudia Elimu Bure ikitolewa kuanzia elimu ya msingi mpaka sekondari, mikopo ya elimu wakipatiwa wenye sifa satahiki, mishahara na stahiki kwa wafanyakazi vikilipwa kwa wakati. Hakika nchi inasonga mbele.

Sekta za afya, kilimo zikizidi kuwa bora zaidi. Mathalani tumeona ununuzi wa madawa, vitanda na vifaa tiba mahospitalini; wakulima wakinufaika na jasho lao kwa kulipwa bei nzuri na kukomeshwa kwa mtindo wa lumbesa uliokuwa ukiwanyonya wakulima.

Hakika tunaendelea kujivunia amani yetu, upendo, ulinzi na usalama. Hakika Tanzania inazidi kusonga mbele chini ya utawala wa Mhe.Rais Dk. Magufuli.

Na Emmanuel Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top