Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UTAWALA WA RAIS MAGUFULI NI KIBOKO



Tangu tupate uhuru hakuna Rais amewahi fanya hili. Huyu Rais Magufuli sio wa kawaida aisee nchi yote ifunge na kumwombea Rais Magufuli. BOT kwa Mara ya kwanza imeshusha riba za Mabenki kutoka asilimia 16 mpaka asilimia 12.

Hapo awali Benki zilikuwa hazikopi BOT kutokana na riba kuwa Kubwa iliyowalazimu Wananchi kulipa riba ya asilimia 25.

Kutokana na kushuka huku kwa riba ni dhahiri mikopo kwa mabenki itaongezeka na riba kwa Wananchi itapungua.  Nani kama Rais Magufuli?

Hili lina faida Kubwa. Kwanza mzunguko wa pesa unakwenda kuwa mkubwa. Msamiati wa pesa kupotea mitaani hautakuwepo tena.

Inakwenda kuchochea uchumi kwa kuongeza uwekezaji kwa sababu wengi watakopa na hivyo mzunguko wa pesa kuwa mkubwa.

Pia itasaidia kudhibiti mfumuko wa bei ya bidhaa na huduma unaonyemelea nchi kwa sasa.

Hakika, nchi imerudishwa kwa Watanzania wanyonge.

Mungu Mbariki Rais Magufuli.
Mungu ibariki Tanzania

Na Emmanuel John Shilatu
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top