Wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wamechukuliwa hatua za kinidhamu kufuatia kurusha habari ya uongo kuhusu Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kufuatia kurusha taarifa ya uongo kutoka tovuti ya fox-channel.com ambayo ilidai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mkubwa na vita dhidi ya dawa za kulevya. Tovuti halali ya Fox ni foxnews.com na si hiyo iliyonukuliwa na TBC.
Mkurugenzi wa TBC, Dk. Ayoub Riyoba amethibitisha kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa wafanyakazi hao kufuatia kosa hilo walilolifanya.
“Ni kweli watu kadhaa wamesimamishwa kazi kutokana na suala hilo.”
Wafanyakazi tisa waliosimamishwa ni pamoja na Elizabeth Mramba, Gabriel Zacharia, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.
==>Hii ndo taarifa ya uongo iliyosomwa TBC.
Post a Comment