Waziri wa Fedha na Mipango Mh.Philip Mipango amesema Bungeni kuwa kwa mwaka ujao wa fedha serikali itaongeza bajeti ya mfuko wa Bunge kutoka shilingi bilioni 99 mpaka shilingi bilioni 121.
Mh. Mipango ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mh. Lucy Magereli mbunge wa viti maalum aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuliwezesha bunge ili liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Akaongeza kuwa mpango wa serikali kuliwezesha bunge kufanya shughuli zake kwa ufanisi ni kutoa mfuko mkuu wa serikali kwenda kwenye mfuko wa bunge kwa kuzingatia bajeti iliyoidhinishwa na bunge .
EU Laonya Vikwazo Vya Marekani Dhidi Ya ICC
1 hour ago
Post a Comment