Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Makonda awapa siku 10 wauza CD Dar

RC PAUL MAKONDA
Hatua hiyo imefuata baada ya kundi la wasani wa 'Bongo Movie' likiongozwa na Jacob Steven- JB kufika ofisini kwake na kumueleza namna ambavyo baadhi ya Watanzania wenye maduka ya filamu kutoka nje ya nchi yanavyochangia kuua tasnia ya Filamu Tanzania.
Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda  (katikati) akiwa Kamanda Siro kwenye Picha ya Pamoja na Baadhi ya Wasanii waliofika Ofisini hapo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda amepiga marufuku kuanzia Alhamisi hii tarehe 06 Aprili, 2017 uuzwaji, uingizwaji wa filamu za nje ambazo hazina stika za TRA ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Aidha amesema baada ya siku kumi ofisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa wamekiuka agizo hilo.

Amesema hayo amapema leo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kutembelewa na wasanii wa filamu wakiongozwa na Jacob Stephan wakilalamikia kuzagaa kwa kazi zao ambazo zimedurufiwa na wafanyabishara wasiowaaminifu.

Akiongea na waandishi pamoja na wasanii hao, Mh Makonda aliwaagiza watu wa bodi ya filamu kufanya tadhmini ya haraka kubaini ni maduka mangapi yanayouza mikanda ya filamu jiji Dar es Salaam.

Wasanii hao pamoja na wasambazaji walidai hawanufaiki na kazi zao za filamu kutokana na kuwepo kwa maharamia wanaoziiba kazi hizo kwa kuzi-download kisha kuzisambaza kimagendo kwa bei ya kutupa bila ridha yao na zikiwa hazina stempu ya mamlaka ya mapato.

Wasanii wengine ambao walifika ofisini hapo ni pamoja na Ray Kigosi, Odama, Tino, Jimmy Mafufu pamoja na wasambazaji wa filamu.

TAZAMA VIDEO HAPO CHINI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top