Na Waandishi Wetu, Dar na Dodoma
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wasomi mbalimbali nchinmi wameeleza kushangazwa na chama cha upinzani nchini, Chadema, kushindwa kuenzi demokrasia na misingi ya haki kufuatia chama hicho kuwasilisha majina ya wagombea wawili tu katika nafasi zao mbili za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Dodoma na wabunge hao na wasomi wengine mbalimbali wakati wa Mahojiano Maalum na Mwandishi wa habari hizi kuhusu uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika jana Mjini Dodoma.
Akizungumzia kuhusu Uchaguzi huo Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Amina Mollel alisema Bunge la Tanzania kama yalivyo Mabunge mengine duniani yameendelea kuzingatia suala la usawa wa kijinsia, na hivyo hatua ya Wabunge wa CHADEMA waliokuwa wawili tu katika nafasi mbili kukataliwa ilikuwa ni sawa.
Katika majina ya Chadema, hakukuwa na uwakilishi wa kijisia wala pande mbili za Muungano, ambapo badala yake, wagombea wote wa chama hicho walikuwa wa jinsia moja na kutoka mkoa na wilaya moja.
Mbunge Mollel ameongeza kitendo kilichofanywa na CHADEMA ni kukiuka kanuni za Bunge hilo na la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo yote kwa pamoja yamesisitiza suala la usawa wa kijinsia katika nafasi za uteuzi wa Chombo hicho cha kutunga Sheria.
“Serikali ya awamu ya nne ilijitahidi sana katika kusimamia suala la usawa wa kijinsia kwa kuwa hata katika maazimio ya Mkutano wa Wanawake uliofanyika Jijini Beijing China mwaka 1995 ulizitaka nchi zote ulimwenguni kuheshimu haki na usawa wa wanawake” alisema Mhe. Mollel.
Mhe. Amina Mollel:Sijawaelewa kabisa Chadema. |
Aliongeza kuwa pamoja na idadi kubwa ya wagombea waliofikia 400, CCM ilipata majina ya wagombea 12 kuwania nafasi sita hatua iliyodhirisha kuwa Chama hicho kimekomaa kisiasa tofauti na vyama vingine vya upinzani vilivyopo nchini.
Naye Mbunge waSingida Mjini (CCM) Musa Sima aliwapongeza Wabunge wapya wa Bunge la Afrika Mashariki na kusifu ukomavu wa kisiasa ulionyeshwa na Wabunge wa Bunge la Tanzania wakati wa mchakato wa uteuzi wa Wabunge.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeomba jina lake lisiwekwe hadharani akiwa na ngazi ya cheo cha Profesa ametabiri kuzidi kutokea kwa hatima ya Chadema katika siasa za kitaifa.
“Ni chama ambacho kinadidimia. Kila siku ukitazama misingi ya kuanzishwa kwake, sera zilizowafanya kuwepo walipo na sababu za kufika walipo zote wameanza kuzisigina,” alisema msomi huyo aliyebobea katika sayansi za siasa.
Mbunge wa Viti Mary Mwanjelwa amelisifu Bunge kwa kusimamia sheria na kanuni katika uchaguzi huo akisema isingekuwa vyema kwa chama kimoja kuteua watu na kutaka wapite bila kupingwa badala ya kushindanisha wagombea husika.
"Siamini kama hiki ndio chama walichokipigania akina Mbowe, Slaa, Mnyika, Lissu, Mdee na wengine. Kuna tatizo. Nadhani wamefikia mwisho wa kufikiri," anasema mwanafunzi wa sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe, Johnson Minaeli.
Post a Comment