Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Zitto Kabwe aanikwa



Nimemsikiliza Zitto Kabwe wakati akichangia bungeni asubuhi kuhusu matukio ya watu kutekwa na kupigwa. Moja ya matukio aliyozungumzia ni kuvamiwa kwa mwandishi Absalom Kibanda.

Zitto amelitaka bunge kuunda Kamati maalum kuchunguza mambo hayo ambayo kwa mchango wake anaonekana kuyahusisha moja kwa moja na serikali.

Nimkumbushe Zitto kwamba, tukio la kuvamiwa Kibanda lilitokea baada ya yeye kuandika makala kuwatadharisha wapinzani hasa Chadema, kuhusu ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana.

Makala hiyo ilikuwa na kichwa cha habari; "Namuogopa Abrahman Kinana". Ndani ya makala hiyo alielezea sifa za Kinana kisiasa na kuweka wazi kwamba, haziwezi kufananishwa na viongozi wa upinzani akiwemo Slaa ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa Chadema.

Makala hiyo Kibanda aliandika akiwa Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, linalomilikiwa na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wakati huo Chadema walikuwa kwenye mashambulizi dhidi ya Kinana baada ya kukabidhiwa 'mikoba' ya ukatibu mkuu wa CCM.

Baada ya makala hiyo, Kibanda akaondoka Tanzania Daima, inadaiwa ni baada ya kutokea kutoelewana na wakubwa wake.

Haikuchukua muda mrefu Kibanda akahamia gazeti la Mtanzania, hakukaa muda mrefu akavamiwa na kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana.

Nakumbuka moja ya maandiko yake baada ya kupata nafuu, nanukuu sehemu mojawapo; "Hakuna vita ngumu kama ile ya kutomjua adui yako au ile ambayo mtu au watu uliowaona kuwa ndugu na marafiki wanapogeuka kwa njia ya siri kuwa maadui wanaoamini katika kisasi chenye adhabu ya kifo kwa kosa la kuwakosoa tu".

Zitto Kabwe na kila anayesoma hapa aitafakari kauli hii ya Kibanda. MUNGU IBARIKI TANZANIA!!
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top