Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimemsimamisha uanachama aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho upande wa Zanzibar, Ramadhan Ramadhan kutokana na kukaidi adhabu ya onyo aliyopewa na viongozi wa chama hicho.
Hatua hiyo inatokana na msimamo wa kiongozi huyo kushiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, mwaka jana pamoja na kumtambua Rais Dk. Ali Mohamed Shein.
Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa chama hicho, Abdallah Khamis ilieleza, uamuzi wa kusimamishwa uanachama kwa kiongozi huyo umetolewa kwenye kikao cha pili cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika Mei 7, mwaka huu mjini Kahama.
Alisema kutokana na hali hiyo, kikao hicho kilimteua Juma Saanani ambaye alikua Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kutoka Zanzibar, hadi suala la Ramadhan litakapoamuliwa na Halmashauri Kuu ya chama hicho.
“Uamuzi wa kusimamisha uanachama Ramadhan ulikuja baada ya kamati kuu ya chama chetu kubaini kuwa aliwahi kukutwa na makosa mbalimbali na Kamati ya chama ya Uadilifu,” alisema Abdallah.
Kutokana na hali hiyo kamati hiyo iliamua kumpa adhabu ya onyo kali na kumtaka kutorudia makosa yake ambayo ni pamoja na kupingana na msimamo rasmi wa chama wa kutoutambua na kutoshiriki kwenye uchaguzi batili wa marudio wa Zanzibar uliofanyika Machi 20, 2016 lakini alikaidi.
Alisema pia, aliwahi kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa chama hicho kinamtambua na kumuunga mkono Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kinyume na matamko rasmi ya Chama.
Rais Samia apongezwa kuwezesha ujenzi ofisi kuu za WMA
39 minutes ago
Post a Comment