Jana tarehe 02, Mei 2017 tumekuwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Mh. Humphrey Polepole ambaye amefanya ziara ya kukiimarisha chama chetu cha mapinduzi CCM katika wilaya yetu ya Longido na kuzungumza na wanaCCM wakiwamo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Longido, wajumbe kamati ya siasa ya wilaya.
Mh. polepole amesema yafuatayo:
1. Serikali imedhamiria haswaa kuimarisha sekta ya usafiri wa anga ( ATCL ) kwa kuagiza ndege zingine ili kufikia ndege saba ikiwamo ndege kubwa ya kubeba abiria wasiopungua300, ndege tatu zenye uwezo wa kubeba abiria 102 kila moja ambazo zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini ili kuliingizia taifa fedha za kigeni.
2. Serikali italeta kwa wananchi tani 500 za chakula kwa bei nafuu ili kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kumudu bei za chakula sokoni. kwa mujibu wa mheshimiwa Polepole Chakula hicho kitaanza kuingia juma lijalo.
3. Tutapambana kufa na kupona ili kurejesha ccm jimbo la longido na kata zake zote zilizobebwa na wapinzani.
4. Mradi mkubwa wa maji kusainiwa tarehe 06/05/2017 ili kuwaletea wanachi wa longido huduma ya maji na kuwaondolea kabisa shida ya maji na tatizo kuwa historia. Mradi huo utatoa maji kutoka West Kilimanjaro wilaya ya Siha.
5. Kiwanda kikubwa haswaa cha kutengeneza viatu kujengwa moshi Kilimanjaro na kwamba wamasai sasa wajiandae kupata soko kubwa la ngozi ya ng’ombe zitakazohitaji katika kiwanda hicho.
6. Chama cha mapinduzi kimepanga kujenga chuo kikubwa cha uongozi kwa ajili ya wanaccm na kwamba yeyote mwenye ndoto ya kuwa kiongozi ni lazima apitie chuo hicho.
7. Mheshimiwa Polepole ameguswa na Changamoto mbalimbali zinazoikabili CCM Longido ikiwamo Kukosa Ofisi ya Chama yenye kukidhi mahitaji ya sasa na hivyo Kuchangia Tsh. 500,000/= kwa ajili ya Shughuli za Ujenzi. Tuungane pamoja kukijenga Chama.
8.Mheshimiwa Polepole ametoa rai kwa Wanaccm kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa ndani wa Chama cha mapinduzi unaendeleaje nchini kote. Ametutaka tuchague viongozi wenye mapenzi mema na nchi yetu na Taifa kwa Ujumla, wenye vigezo stahiki & Waadirifu. Tusiwape nafasi Watoa rushwa ambao hutumia pesa zao kusaka uongozi. Hili halikubaliki hata kidogo.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi...Hii ndiyo ccm bwana, tukiahidi tunatekeleza. HAPA KAZI TU.
Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM (M) Arusha.
Mei 02, 2017
Post a Comment