Dar es Salaam. Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu na wanaovunja matakwa ya sheria katika uingizaji, usafirishaji na uhifadhi wa kemikali.
Hayo yamesemwa leo na Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele wakati alipozungumza na wanahabari kuhusu kampuni ya Techno Net Scientific kukutwa na kemikali bashirifu bila usajili.
Amesema ofisi yake ilitoa usajili wa muda wa miaka miwili kwa kampuni hiyo ambao uliishia Aprili 30 mwaka 2016 lakini bado ikawa inaendelea na shughuli zake kinyume cha sheria.
Profesa Manyele alibainisha kuwa kampuni hiyo imebainika kwamba imekuwa ikiingiza kemikali nchini kwa kutumia njia za udanganyifu na vibali vya bandia.
Loading...
Post a Comment