Baada ya kufanikiwa kuondoka Tanzania May 14, 2017 kwenda Marekani kwaajili ya matibabu hatimaye watoto watatu waliochukuliwa na ndege ya Samaritans Purse wamewasili salama nchini humo asubuhi ya leo May 15, 2017.
Kwa mujibu wa Mbunge Lazaro Nyalandu ambaye amekuwa karibu sana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa ameeleza kuwa ndege hiyo imefika mji wa Charlotte NC, Marekani na majeruhi hao wamepelekwa Hospitali ili kuimarishwa kiafya.
Baada ya hapo watachukuliwa na ndege nyingine maalum na kupelekwa hospitali ya Mercy iliyopo Sioux City jimbo la Iowa kwaajili ya huduma ya matibabu kamili.
Watoto hao watatu walinusurika kwenye ajali ya basi iliyoua wanafunzi wenzao 33, walimu wawili na dereva wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha wiki iliyopita.
Post a Comment