Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia baolake ambalo lilikuwa ni pekee katika mchezo wao dhidi ya wadogo zao Toto Africa wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa Amis Tambwe katika dakika za mwisho za mchezo huo.
Kwa ushindi huo sasa Yanga wamejihakikishia ubingwa baada ya kufikisha jumla ya Pointi 68 ambazo wapinzani wao Simba hata wakishinda mchezo wao uliobaki bado Yanga watakuwa wakibebwa ba wastani mkubwa wa mabao ya kufunga huku wakiwa bado wana mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Amis Tambwe akifunga bao hilo katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkubwa
Nahodha Niyonzima akimpongeza Amis Tambwe baada ya kutupia bao hilo
Shabiki wa Yanga akishngilia kwa staili ya kula Samaki mara tu baada ya Tambwe kutupia bao hilo. Shabiki huyu huwa na staili tofauti tofauti za kushangilia kulingana na timu inayo kuwa ikicheza dhidi ya timu yake ya Yanga, ambapo majuzi aliibuka uwanjani hapo akiwa na Mahotpot mawili yakiwa na kipolo cha ubwabwa maharage, siku za nyuma alishaibuka uwanjani hapo akiwa na Msumeno wakati Yanga ikicheza na Mbao Fc na nyinginezo,
Chirwa akipambana na mabeki wa Toto African
Gooooooooooooooo
Hatari langoni kwa Toto African
Deus Kaseke akichuana na beki wa Toto African
KIpa wa Toto African akiruka kupangua mpira wa hatari langoni kwake...
Mashabiki wa Yanga wakiwa katika sare maalum kuomboleza kifo cha shabiki mwenzao
Wachezaji wa Yanga wakishangilia
Credit: Mafoto blog
Post a Comment