Watumishi zaidi ya sabini wamesimamishwa kazi wilayani Misungwi Mwanza kwa kukutwa na vyeti feki, ubadhilifu wa mali za Umma na utovu wa nidhamu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi Bw. Athon Masele amesema kuwa watumishi 68 wamekutwa na vyeti feki, wawili walikuwa ni wabadhilifu wa mali za Umma huku wengine wawili walikuwa ni watovu wa nidhamu, jambo ambali limepelekea idara ya elimu na afya kuathirika kwa kiwango kikubwa zaidi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mh. Charles Kitwanga amesema mwaka jana walisimamishwa kazi watumishi wawili kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali za umma ambapo katika kipindi cha mwezi mmoja mapato yameongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka kiasi cha shilingi milioni 24 hadi shilingi milioni 120 kwa mwezi hali iliyosaidia kupata hati safi baada ya CAG kuridhishwa na utendaji kazi wa halmashauri
Post a Comment