Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri Mwijage awatangazia vita watumishi wa umma

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametangaza vita kwa watumishi wanaoruhusu uingizwaji wa bidhaa bandia nchini, na kutoa onyo kwamba watakao fanya hivyo wajiandae kuondoka.   

Mwijage ametoa onyo hilo juzi Bungeni mjini Dodoma, wakati akisoma bajeti ya wizara yake, ambapo pia alipiga marufuku bidhaa bandia kuingia nchini kutoka nje ya nchi kuanzia Julai mosi mwaka huu.

“Ikifika mwezi Julai mwaka huu, kama bidhaa feki zikipita kuingia nchini mtakuwa hamnitakii mema, na walio chini yangu mkae kabisa mkao wa kuondoka kama bidhaa zisizokidhi viwango zitapia na kuja kuumiza viwanda vyetu nchini,” alisema.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top