Baada ya kuanua matanga ya mumewe, Ivan Ssemwanga ‘Don Ivan’ aliyefariki dunia Mei 25, mwaka huu na kuzikwa huko Nakalilo nchini Uganda, staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ameondoka nchini humo na kuelekea nchini Afrika Kusini akiwa na wanaye hao wa kiume aliozaa na jamaa huyo, Pinto, Raphael na Quincy.
Akizungumza na mtandao wa habari za udaku wa Kampala muda mfupi kabla ya kukwea pipa, Zari alisema kuwa, watu wanadhani atashindwa kuwalea watoto hao wa Ivan kwa kuwa ana wengine wawili aliozaa na mwanaume wake wa sasa, lakini si kweli kwani ana uhakika wa kuwalea watoto hao.
“Watu wanasema nitaweza? Wengine wanasema siwezi? Hapana, naweza. Siwezi kushindwa kuwalea wanangu, nitawalea mwenyewe,” alikaririwa Zari.
Baada ya kuondoka nchini Uganda, Zari alikwenda moja kwa moja na wanaye na kuweka makazi kwenye nyumba aliyonunua mpenzi wake wa sasa iliyopo jijini Johannesburg.
Post a Comment