KIBITI, PWANI: Watu 3 wakazi wa kijiji cha Nyamisati wafariki baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo
Watatu wauawa kwa kupigwa risasi Kibiti
Mkazi mmoja wa Kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza amesema miongoni mwa watu waliopigwa yumo mwanamke mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji kimojawapo kijijini hapo.
KAMANDA WA PWANI AFAFANUA MAUAJI YA WATU WATATU
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema kwa taarifa alizonazo, watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati, Kibiti, kisha waliofanya uhalifu huo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao.
Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo.
Watu watatu, wanahofiwa kuuawa kwa kupigwa risasi wilayani Kibiti usiku wa kuamkia leo. DC wa Kibiti Gullamhusein Kifu amesema
Chanzo: JF na Mwananchi
on Friday, June 9, 2017
Post a Comment