Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewasilisha bajeti yake iliyopewa jina la mageuzi ya Trilioni moja ambapo hakuna kodi mpya ingawa itafanya marekebisho ya kuondosha baadhi ya kodi za Muungano na kuzigeuza kuwa za serikali ya Zanzibar.
Akisoma bajeti hiyo katika ukumbi wa Baraza la wawakilsihi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Khalid Mohamed amesema serikari haitoanzisha kodi mpya yoyete na kodi zitabaki pale pale ingawa itaongeza nguvu zake kwenye vyanzo na kufanya marekebisho ya kodi za Jamhuri ya Muungano zinazotumika Zanzibar.
Dkt Khalid pia alizungumzia ujenzi wa uwanja wa ndege mpya wa Zanzibar ambao umekwama na umekuwa ukilalamikiwa na wajumbe na wananchi ambapo amesema matatizo yake yamekwisha na ujenzi wake unatarajiwa kuendelea mwaka huu wa fedha na serikali inafahamu kuwa huo ni moja ya mlango mkubwa wa pato la serikali.
Waziri wa Fedha Dkt Khalid pamoja na kusema hapatakuwepo na ongezeko la kodi lakini amesema kuanzia mwaka ujao wa fedha itapndisha ada ya usajli wa namba binafsi za magari kutoka shilingi Milioni tatu kwa miaka mitatu na sasa itakuwa milioni 15 kwa mwaka,hata hivyo amewahakiksihia wastaafu wote wa serikali itapandisha kiwango cha pensheni yao mwaka huu.
Waziri wa Fedha aliomba Baraza kuidhinisha shlingi trilioni moja,bilioni 87 na Milioni 400 kwa ajili ya makadirio na mapato na matumzi kwa mwaka 2017/2018.
Loading...
Post a Comment