Said Mrisho
UKIMWAGA mboga, mimi namwaga ugali! Siku moja baada ya kuripotiwa kwa habari ya kufumiwa na mkewe wa ndoa, jamaa anayedaiwa kutobolewa macho katika tukio lililoteka hisia za wengi, Said Mrisho amefunguka na kuweka wazi maizngira yote ya fumanizi hilo, haraka sana teremsha macho hapa chini.
Katika mazungumzo muhimu (exclusive) na Global Publishers,namba moja kwa habari zenye kushtua, Said alikiri kukumbwa na kazia hiyo kwa kile alichokiita, “mitihani ya akibinadamu…” na kueleza kuwa amemvumilia mengi mkewe huyo (Stara Soud) hivyo kuamua kunyanyua mikono hivyo kuishi na mwanamke anayeamini ndiye sahihi kwa sasa.
“Mwanamke ninayeishi naye kwa sasa, nilimuoa zamani lakini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri sana, ndiyo maana sikuwa naishi naye lakini hata Stara nilishamwambia kuwa simtaki, cha ajabu akawa haelewi na matokeo yake ndiyo kama ilivyotokea,” alisema Said na kuongeza;
“Kuhusu watoto si kweli kwamba nimewatelekeza wale bado ni wadogo sana na sheria hainiruhusu kuwachukua, muhimu ni kwamba nitakuwa nahudumia na ndiyo maana nimempangia nyumba akae na wanangu ili wasipate tabu, hayo mengine yanabaki maneno yenye lengo la kupotosha uhalisia,” alisema Said.
Tukio la Said kutobolewa macho linatajwa kujiri mwaka jana maeno ya Buguruni-Sheri jijini Dar kwa kile kilichoelezwa akiwa katika manunuzi ya baadhi ya vitu kabla ya kuvamiwa na mtuhumiwa anayetajwa kama Scorpion na kesi hiyo kuwa mahakamani hadi sasa.
“Mke wangu nimemuacha sababu ya tabia zake mwanzoni nikiwa naona alikuwa akinisaliti lakini hata sasa anaendelea kunisaliti. Siku moja aliniomba simu akaniambia anaomba simu ampigie mtu aliyemkopesha Pesa hospitali. Nilimpatia simu mama dee na akatoka lakini alichelewa kurudi nikamuuliza vipi akasema alikuwa hapatikani lakini baadaye nikabonyeza button ya kupiga.
Nilipopiga simu akapokea mwanaume mwingine nikamuuliza vipi akaniambia huyu ni mke wake kivipi wakati ni mke wangu mimi. Japokuwa nimepata zile bajaji huwezi kuamini navyonyanyasika kwenye familia yao hata hesabu za siku hawaleti.”
Source: Global Publisher
Post a Comment