Askari wa usalama barabarani "trafiki" mkoani Tabora amefariki dunia baada ya kugongwa na gari wakati akitekeleza majukumu yake. Askari huyo aliyefahamika kwa jina E.51 Koplo Aswile Ambwene amefariki dunia leo asubuhi ya saa 12:30 akiwa kazini eneo la barabara ya Sikonge, kijiji cha Kipalapala kwa Chief, kata ya Itetemia, mkoani Tabora.
Mauti ya askari huyo yamesababishwa na gari lenye namba za usajili 564 ALG aina ya Isuzu likiendeshwa na dreva Hasan Husein-Kiula mwenye umri wa miaka 36. Gari hilo lilikuwa likitokea Mpanda kwenda Kahama likiwa limepakia magunia ya mahindi.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo anaeleza kuwa Bwana Hasan(dreva wa gari hilo) alisimamishwa barabarani na askari mwenye namba G.4246 Konstebo Abuu ndipo dreva huyo aligoma kusimama na kupelekea kumgonga askari namba E.51 Koplo Aswile Ambwene ambaye alipoteza maisha papo hapo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Milambo Jeshini mkoani Tabora
Post a Comment