Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili Makao Makuu ya Polisi kwa ajili ya mahojiano na Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz.
Lowassa amewasili saa 3:05 akiwa ameambatana na Wakili wake, Peter Kibatala ambao wamekuja na msafara wa magari matatu.
Kama ilivyokuwa wakati anahojiwa siku ya kwanza Juni 28, ulinzi umeendelea kuimarishwa huku waandishi wa habari wakifukuzwa.
Hii ni mara ya tatu kwa Lowassa kwenda katika ofisi za DCI ambako anahojiwa kwa tuhuma za uchochezi.
Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alihojiwa Juni 28 na Juni 29. Wakili Kibatala aliwaeleza wanahabari kuwa Lowassa anadaiwa kutoa maneno ya kichochezi Juni 23 katika futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.
Tutaendelea kukujuza kuhusu mahojiano ya Lowassa kwa DCI.
Post a Comment