Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mameneja 6 NSSF Wapigwa chini

Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) imewaachisha kazi wafanyakazi 12 waliokuwa wamesimamishwa kwa mwaka mmoja sasa.

Wafanyakazi hao walisimamishwa kazi Julai 2016 kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi.

Taarifa ya NSSF iliyotolewa leo Alhamisi (Julai 13) kupitia vyombo vya habari walioachishwa kazi ni Yacob Kidula, aliyekuwa mkurugenzi wa mipango, uwekezaji na miradi.

Wengine na nafasi walizokuwa wakishikilia kwenye mabano ni Ludocick Mrosso (mkurugenzi wa fedha), Chiku Matessa (mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala), Sadi Shemliwa (mkurugenzi wa udhibiti, hadhara na majanga), Pauline Mtunda (mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za ndani).

Crescentius Magori (mkurugenzi  wa uendeshaji), Amina Abdallah (meneja utawala), Abdallah Mselli (meneja wa uwekezaji), Mhandisi John Ndazi (meneja miradi), Wakili Chedrick Komba (meneja kiongozi Mkoa wa Temeke) na Ramadhani Nassibu (meneja mkuu usalama).

-MCL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top