Emmanuel Mbasha.
Mbasha aliandika ujumbe huo kama majibu, baada ya hivi karibuni kusambaa kwa taarifa ambazo si za kweli zilizodai kuwa Flora alifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio na kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Mbasha, akisema uvivu wake kitandani ndiyo chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yao, ambapo Flora alikanusha vikali taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Flora Mbasha ‘Madam Flora’.
Baada ya taarifa hizi kutua mezani kwa Emmanuel, alipiga kimya kwa muda kutokana na kuwa bize na msiba wa bibi yake, lakini baada ya mazishi, akaingia kwenye mahakama ya mastaa , Instagram na kuandika ujumbe huu.
“Sipendi ujinga kabisa kwani hamuwezi kuuza hicho kidaftari chenu mpaka mtafute kiki kwangu?, acheni hizo mnaniingiza kwenye upumbavu wenu ili mkiuze hicho kidaftari chenu, Mbona wengine wanauza vyao kwa utaratibu mzuri, sipendi kabisa mie naingiaje kwenye hizo ishu za huyo mwanamke miaka zaidi ya 3 siko nae, na ni mke wa mtu na wewe hembu tulia na mmeo huko tena ukome kunitajataja.
Huoni hata haya eti unakiita kidaftari jina langu si uite la mumeo huyo, kunitajataja tu, taja jina la huyo bwana ako sijui nani vile! asinihusishe, usinihusishe Mnikome mbona mie siwafatili na bwana ako kwa lolote lile, kila mtu apambane na hali yake, pambana na hali yako,” alisema Mbasha.
Alichokiandika Mbasha;
Post a Comment