Muuguzi wa Kituo cha Afya Kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Damian Samson Mguya (26) amesimamishwa kazi na kufutiwa leseni yake ya uuguzi kwa tuhuma za kumbaka ndugu wa mgonjwa baada ya kumuwekea dawa za kulevya.
Kufuatia kitendo hicho Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imelaani kitendo ambacho muuguzi huyo amekifanya na kutaka leseni ya muuguzi huyo kusitishwa mara moja kwa kukiuka taratibu na kanuni za uuguzi.
Aidha msemaji wa Idara Kuu ya Afya, Nsachris Mwamwaja amewataka watumishi wote wa sekta ya afya nchini kuhakikisha wanafuata kanuni, utaratibu na maadili ya taaluma zao muda wote na siku zote.
Muuguzi Damian Mguya anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kumbaka binti wa miaka 18 mkazi wa Kijiji cha Mwagala, ambaye aliongozana na mgonjwa kwenda katika kituo hicho cha afya, upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika muuguzi huyo atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.
Post a Comment