Watu wasiojulikana wanadaiwa kumuua kwa kumpiga risasi, mkazi wa Kijiji cha Ruaruke, wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani Ramadhani Mzurui, usiku wa kuamkia leo.
Kadhalika watu hao walimjeruhi mguuni kwa risasi mke wa marehemu.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Mchukwi, Dk Emmanuel Humbi amethibitisha kufikishwa hospitalini hapo kwa mwanamke huyo akiwa na majeraha ya kupigwa risasi na kusema kwa sasa yupo katika chumba cha matibabu ya dharura.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema tayari polisi wamekwenda eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.
Post a Comment