UZINDUZI NYUMBA 50 ZA WATUMISHI WA AFYA ZILIZOFANYIKA MKOANI CHATO
Leo Jumatatu Julai 10, 2017 Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa amekabidhi nyumba 50 kupitia taasisi yake ya mkapa Foundation kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, John Magufuli.
-Nyumba hizo ni kwa ajili ya watumishi wa afya kwa mikoa ya Geita, Kagera na Simiyu na hafla inafanyika Chato.
NUKUU MUHIMU:
"Asilimia 28 ya Watanzania wanatumia bima za Afya" - Waziri Ummy
"Wakurugenzi wawakatie Wazee bima za afya na wawape vitambulisho vya utambuzi wa matibabu bure. Mwisho wa agizo ilikuwa tarehe Juni 30" - Waziri Ummy
"Mwezi ujao Rais Magufuli atazindua huduma ya kupandikiza figo hapa nchini ndani ya hospitali ya Muhimbili. Hii haijawahi kutokea hapa nchini" Waziri Ummy
"Hakuna Mwanamke mjamzito atakaye kufa kwa kukosa sindano ya kuzuia damu au dawa ya kuzuia kifafa cha mimba katika utawala wa Rais Magufuli" - Waziri Ummy
"Muda wa kuishi Watanzania umeongezeka kutoka miaka 51 hadi kufikia miaka 61" - Waziri Ummy
"Mwaka 2005 kulikuwa na vituo vya afya 4000 na sasa kuna vituo vya afya zaidi ya 7200 vinavyotoa huduma bora za kiafya" - Waziri Ummy
"Vifo vya Watoto wachanga chini ya mwaka mmoja vimepungua kwa asilimia 50" - Waziri Ummy
"Takwimu alizotoa Waziri wa Afya juu maendeleo ya afya naamini itapunguza kidogo 'Upumbavu' wa wale niliowaita wapumbavu" - Benjamin Mkapa
"Niliagiza dawa zishuke bei na zimeshuka kweli kupitia agizo nililowapa la kununua dawa moja kwa moja zinapotengenezwa" - Rais Magufuli
"Bajeti ya dawa ya mwaka huu 2017/2018 imeongezeka kutoka Bilioni 31 hadi Bilioni 200" - Rais Magufuli
"Serikali ninayoiongoza siku zote nitakuwa na Wanyonge" - Rais Magufuli
"Tangu niingie nafuta kodi zote zinazowabana wanyonge. Nimefuta kodi 80 za kilimo, kodi 7 za mifugo, kodi 5 za uvuvi, kodi 30 za kwenye kahawa, kodi zote za Pamba na Korosho. Pia kusafirisha tani moja ya chakula kutoka wilaya moja kwenda nyingine ni bure" - Rais Magufuli
"Serikali haiwezi kufanya biashara na Maskini na kuwaacha Matajiri" - Rais Magufuli
"Hatujazuia Watu kuchimba madini, lakini wachimbe watupe na faida ya kodi zetu" - Rais Magufuli
"Nililetewa miswada ya marekebisho ya sheria za madini tarehe Julai 7 na siku hiyo hiyo nikazisaini" - Rais Magufuli
"Sio Watoto wote wanapata mimba kwa kubakwa, sisomeshi Wazazi" - Rais Magufuli
"Tunafanya uhakiki wa pembejeo za kilimo. Tumegundua mpaka sasa madai ya pembejeo ya Tsh. Bilioni 50 zilizowasilishwa, Bilioni 8 ndio madai halali" - Rais Magufuli
Imeandaliwa na:
Emmanuel J. Shilatu
10/07/2017
Post a Comment