Loading...
Shaka ashtukia mchezo mchafu UVCCM
Zipo taarifa zenye ushahidi wakina kwamba wako watu wanaomaliza muda wao wa uongozi katika jumuiya yetu wameanza kupanga safu nani achukue fomu wapi na nani achukue fomu wapi.
Naendelea kuwakumbusha ndugu zangu kuwa anayetaka kupanga safu aende akapange nyanya sokoni na si uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake. CCM ina hazina ya kutosha ya vijana ambao wanaweza kuwa viongozi.
Anaepanga na anaepangwa wakibainika wote watakula panga haiwezekani mtu mmoja kujifanya ana hati miliki ya chama au jumuiya akaanza kupangia wenziwe safu ya uongozi.
Msiogope vijana jitokezeni kwa wingi kuomba nafasi hakuna aliyeandaliwa kushika wadhifa fulani ndani ya jumuiya hii, chama chetu kina demokrasia pana sana tumieni haki na wajibu wenu wa kikanuni na kikatiba.
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
01/07/2017
KAIMU KATIBU MKUU UVCCM
Post a Comment