Na Mwandishi Wetu, Kigoma
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umewataka Vijana wa Tanzania kufanyakazi kama wafanyavyo siafu au wanavyoishi vijana wa kichina wanvyojituma kwa bidii kufanya kazi kwa na kuyakwepa maisha ya utegemeze, uvivu au kukata tamaa.
Pia umoja huo umeelezea haiba ya uhuru, kujitawala wenyewe, demokrasia, amani na utulivu hautaweza kuleta maana yoyote ikiwa wananchi katika Taifa husika hawafanyi kazi na kuzalisha mali.
Kaimu katibu mkuu wa uvccm shaka hamdu shaka aliyaeleza hayo wakati alipozungumza na wanachama wa ccm na jumuiya zake, viongozi wa matawi, kata, wilaya ya kibondo na makundi ya vijana kikao kilichofanyika ukumbi community mkoani hapa.
Shaka alisema dhana ya kujitawala wenye baada ya kuwaondosha wakoloni na wananchi kuwa uhuru, kuendesha utawala kwa njia na misngi ya demokrasia , bila watu kujituma, kufanya kazi za uzalishajo mashambani, viwandani na maofisini, hakutakuwa na faida wala maslahi bila watu kuitisha maisha bora.
Alisema dhamira kuu na msingi kwa waafrika kupigania uhuru na kutaka kujitawala, lengo lilikuwa ni kujitegemea kwa kufanya kazi, wananchi kuwa na maisha bora lakini pia Taifa likijijenga kiuchumi na kimaendeleo.
'Uhuru ,demokrasia na kujitawala hakuna mashiko wala maana ikiwa wananchi wanaojiita wako huru, wakiwa bado wanaombaomba, hawafanyi kazi, hawazalishi, wanapenda ufisadi na baadhi yao bado wana fikra zile zile za kikoloni "Alisema Shaka .
Aidha Kaimu Katibu Mkuu alisema wapo baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambao fikra, mawazo na mitazamo yao ni kutaka kudumaza maendeleo, kuwafanya wananchi waishi kwa unyonge na umasikini.
"Vijana wa Tanzania tuiishi na kufanyakazi kwa pamoja kama wanavyoshirikiana siafu, wenzetu vijana wa China ni hodari kwa kazi na hawapendi tabia za uvivu na utegemezi, wapuuzeni wanasiasa wanaotaka kufubaza maendeleo ya nchi yetu "Alieleza .
Shaka alisema kinachohimizwa na Rais Dk John Magufuli ni kuwataka wananchi wafanye kazi kwa bidii kwani bidii ya kazi humpa tija na manufaa mwananchi mwenyewe lakini pia anawachukia wezi, mafisadi, wabadhirifu wa mali za umma na vibaraka wanaoupigia magoti ukoloni mamboleo.
Kaimu Katibu Mkuu alisema kiongozi aliwataka viongozi na wanachama wa CCM kuhamasisha watu wafanye kazi vijijini na mijini ili kuzalishamali kama njia pekee sahihi ya kuondokana na kadhia ya umasikini .
"Tumekuwa tukihimizwa toka tupate uhuru na kufanyika kwa Mapinduzi ya Zanzibar tuweke juhudi na bidii ya kutokomeza maadui ujinga, umasikini na maradhi, maadui hawa hawatakwisha ikiwa watu hawafanyi kazi"Alisema
Kabla ya kikao hicho cha ndani kufanyika, kiongozi huyo alikutana na wanaCCM katika kata ya Busunzu , kata ya Murungu, kata ya Minyinya kutazama kikundi cha bustan na ushonaji baadae akazindua miradi wa Vijana ya mabwawa ya kufugia samaki katika kijiji cha Minyinya kata ya Bunyambo na kumalizia kijiji cha
Shaka katika msafara wake ameambatana na mbunge wa vijana ccm Zainab Katimba, mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kigoma Peter Msanjira, katibu wa uvccm mkoa wa Kigoma Stephen Koyo na katibu wa wilaya kibondo Pendo Mashija. Kesho ataendelea na ziara yake katika wilaya ya Kakonko na kuhitimisha ziara yake ya siku tano.
Post a Comment