Serikali imeelezea kukerwa kwake na kuendelea kukiukwa kwa agizo ambalo lilitolewa la kuzuia ununuzi wa samani za ofisi za umma kutoka nje ya nchi na badala yake zinunuliwe za hapa hapa nchini.
Waziri wa Fedha na Mipango Dr.Philip Mpango amesema hayo katika viwanja vya maonesho ya biashara vya Mwalimu Julius Nyerere wakati akizungumza na maafisa mbalimbali wa taasisi ambazo zipo chini ya wizara yake.
Katika siku ya kumi ya maonesho hayo ya biashara ya kimataifa ya Dar Es Salaam mamlaka ya maendeleo ya biashara –TANTRADE imeitumia siku hiyo kama siku ya nguo ambapo wadau wanaotengeneza nguo wamekutana na kujadiliana kwa kina kuhusiana na sekta hiyo.
Baadhi ya washiriki wa maonesho hayo wamesema yamekuwa mazuri kwao kwani wameweza kunadi shughuli zao ambazo zimekuwa zikiipunguzia jamii gharama ya maisha.
Post a Comment