Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Waziri wa maliasili na utalii amewapokea mabilionea 28 kutoka mabara yote duniani katika hifadhi ya taifa ya serengeti

Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
amewapokea Mabilionea 26 wa taasisi ya Young Presidents Organisation  (YPO) wakiwa na wenza wao katika Hifadhi ya Taifa  Serengeti kwa ajili ya kutembelea vivutio vya utalii katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.

Mabilionea hao ambao wanatoka katika mabara yote duniani wapo nchini Tanzania kama sehemu ya ziara yao katika nchi 8 duniani ikiwemo Uingereza, Rwanda, Maldives, Nepal, Bhutan na Rajastan.

Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,  Prof. Maghembe aliwakaribisha Tanzania na kwenye Maajabu ya Dunia yanayobebwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Alisisitiza "hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa wanyama wanaokula majani (herbivores) na wale wanaokula nyama (canivores) kama Serengeti".

Prof. Maghembe aliwaeleza Wageni wake kuwa kuhifadhi ni gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia. Hivyo akawaomba wageni hao wawe mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama eneo lenye  amani na vivutio vyenye ubora wa pekee. Hatua hiyo italeta watalii wengi na kuiongezea Tanzania mapato.

Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye uchumi unaokua kwa wastani wa 7% kwa kipindi cha miaka 15 sasa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top