Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amekuja juu na kutoa ya moyoni akionekana kutofurahishwa na taarifa iliyosambaa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandaoni ikitokea Chama cha demokrasia na maendeleo- CHADEMA.
Kauli za Zitto zilifuatia taarifa aliyoiona kwenye ukurasa wa Twitter iliyosema; “CHADEMA waitaka Jumuiya ya kimataifa kuinyima misaada Tanzania kutokana na ukiukwaji wa Demokrasia mfano, kukamatwa kwa viongozi wa upinzani”
Baada ya kuiona hiyo taarifa Zitto Kabwe aliandika “Huu ni uhayawani, hii ni nchi huru, kukaribisha wageni kuingilia mambo yetu ni upuuzi na umazwazwa, tupambane ndani kuleta demokrasia .NDANI”
Baada ya Zitto kuonyesha dhahiri msimamo wake, baadhi ya Followers wake kwenye Twitter walimuandikia kila mmoja na maoni yake na yeye akawajibu kama inavyoonekana hapa chini.
Post a Comment