Msanii wa Bongo Fleva Nchini Ali Kiba amefunguka juu ya siri inayomfanya awe anapata mapokezi makubwa kwa mashabiki wake kila anapotoa kazi mpya kuwa ni kazi nzuri ambazo amekuwa akizifanya.
Akizungumza Juma tatu hii ndani ya ‘Planet Bongo’ya East Africa Radio,Ali Kiba alifunguka kuwa kazi nzuri ndio zinazomfanya awe anapata mapokeo makubwa sana kutoka kwa mashabiki wa muziki wake na wala si kitu kingine kama ambavyo imezoeleka kwa baadhi ya wasanii walio wengi kutumia ‘kiki’ kwa ajili ya kupata mapokeo makubwa ya kazi zao.
‘’Mi nafanya kazi nzuri ndio mana mapokeo ya kazi zangu kwa mashabiki yanakuwa makubwa na sio kitu kingine ninacho kifanya katika kazi yangu zaidi ya kufanya kazi nzuri’’alisema Ali kiba.
Ali Kiba ameanza rasmi kufanya ziara katika vyombo mbali mbali vya habari kwa ajiri ya kuutambulisha wimbo wake mpya ‘Seduce Me’ ambao unatamba sana kwa sasa huku akiongozana na mtayarishaji wa kazi hiyo ‘Man Walter’ kutoka katika studio za Combination Sound.
Post a Comment