Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BREAKING NEWS ... CCM YAFUTA UCHAGUZI KATA 41



Na Mathias Canal, Dar es salaam

Chama Cha Mapinduzi Kimefuta Uchaguzi katika Kata 41 zilizofanya Uchaguzi katika ngazi Mbalimbali kutokana na kukiuka taratibu za  Uchaguzi ikiwa Ni ishara ya Kuelekea kuwa na CCM mpya na Tanzania Mpya.

Kufutwa kwa uchaguzi katika Kata hizo Ni matokeo ya ukiukwaji wa Kanuni za Uchaguzi na katiba ya CCM, kuendeleza makundi baada ya Uchaguzi, Kupanga safu za Uongozi kwa maamuzi ya Nani awe kiongozi Jambo ambalo Ni kinyume na utaratibu wa Uchaguzi.

Akitangaza Kufutwa kwa uchaguzi katika Kata hizo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika Ukumbi mdogo wa CCM wa (OND)-Lumumba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Ndg Humphrey Polepole alisema kuwa hiyo Ni Awamu ya kwanza ya kufanya maamuzi lakini wale wote waliosababisha kadhia hiyo watachukuliwa Hatua kwa mujibu wa taratibu za Chama.

Alisema kuwa wapo wagombea wengine walipokuwa Viongozi katika Awamu zilizopita walishindwa kutoa usimamizi wa Mali za Chama lakini bado wamerejeshwa katika uongozi huku wengine wakiwa si wakazi wa maeneo husika walipoomba nafasi za Uongozi.

Sababu nyingine Ni pamoja na baadhi ya maeneo wajumbe wa vikao kutopewa taarifa sahihi za wagombea Jambo ambalo lilipelekea kuchagua viongozi wasiokuwa na sifa.

Polepole alisema kuwa Kwa mujibu wa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi imetoa mamlaka kwa Katibu Mkuu kutoa Maelekezo ya kufuta Uchaguzi kwa mashauriano na Mwenyekiti wa CCM hivyo kupitia mashauriano Kati ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli na Katibu ya Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Abdulrahiman Kinana kufuta Uchaguzi na kuagiza kurejea upya Uchaguzi huo baada ya kusikiliza malalamiko na kero za kiuchaguzi.

Polepole alizitaka kata hizo kuwa ni Buguruni, Liwiti, Kariakoo, Manzese, Makuburi, Mabibo, Kigamboni, Kiburugwa, Mchafukoge, Gerezani, Segerea, Pugu, Pugu Stesheni, Mianzini, Ndugumbi, Kilungule, Makumbusho, Kitunda, Ukonga, na Msasani katika Mkoa wa Dar es salaam.

Nyingine Ni Kata ya Mapinga iliyopo Mkoa wa Pwani, Kata ya Lumemo Mkoani Morogoro, Kata zote 18 za Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara sambamba na Kata ya Seria iliyopo Kondoa Vijijini Mkoani Dodoma ambayo imefutiwa Uchaguzi wote wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mpanduzi.

Polepole alitoa Rai kwa Viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake kuendelea kusimamia katiba, Kanuni na maadili katika kipindi chote Cha Uchaguzi wa ndani wa Chama kwa kupiga Vita rushwa kadhalika na ubadhilifu wa Mali za umma.

Alisema kuwa CCM inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na kanuni hivyo kama kuna kiongozi atabainika kukiuka taratibu na maadili ya Chama atachukuliwa Hatua ya kuhojiwa na kamati ya maadili na kupitia vikao Hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake.

MWISHO
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top