Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Jerry Muro amtolea uvivu Tundu Lissu

Jerry Muro.

ALIYEKUWA msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amemtolea povu Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu kutaka wanachama wote wa TLS kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili.

Muro ameyaandika haya.

Tundu Lissu, TUNDUNI
Na Jerry C. Muro

Nianze kwa kutoa pole kwa jumuiya nzima ya wanasheria nchini, pole yangu sio ya tukio la IMMA Advocates, bali pole yangu ni ya kuchagua Rais wa TLS chama chenu ‘MAHIRI’ cha wanasheria Tanganyika – TLS Ndugu Tundu Lissu ambae AMEDHIHIRISHA kuwa ameanza rasmi safari ya kuizika TLS, kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusiana na tukio la IMMA Advocates.

Nianze kwa kuweka msingi wa HOJA yangu kuwa sifurahishwi na kilichotokea kwenye IMMA advocates, ila pia SIFURAHISHWI zaidi na “AKILI NDOGO” za Rais wenu katika hatua za AWALI za kushughulikia suala hili.

Mimi ni Profesional communicator kama mwandishi wa Habari, na Nyinyi wanasheria ni Profesional kwenye Sheria, ukisoma na Kusikiliza kwa umakini TAARIFA ya Mhe Rais wa TLS utagundua makosa makubwa sana ya KIUFUNDI ambayo yanaifanya taarifa nzima kuwa kama taarifa ya Mfalme “JUHA” na kwa sisi MAFUNDI wa taarifa tunasema taarifa ikikosewa katika UANDAAJI na UWASILISHWAJI inakuwa imekosa MASHIKO, na hivyo taarifa nzima kuwa BATILI.

KWANINI BATILI

1. Taarifa iliyowasilishwa na Rais wa TLS tayari kwa kiasi kikubwaa ilishatolewa na Chama cha wananchi CUF #teammaalim, ukisoma taarifa ya cuf ambayo ilitoka siku moja kabla ya hii ya Rais utaona nachosema, ila hii ya Rais imewaka mbwembwe ya Vifungu Vifungu vingi vya SHERIA tu, ila taarifa zote zimeonyesha kuwa IMMA advocate ni WABIA katika kazi mana cuf inatetewa na IMMA advocate na Rais Lissu anatetewa na IMMA advocate hivyo wote WANAOMBELEZA DHORUBA YA MMBIA WAO., japo TLS ni Chama na Lissu ni Rais, na ni mteja wa IMMA katika hoja hii ya kwanza nimalizie kwa kusema tu Hoi taarifa ni BATILI kwa kuwa Imekuwa taarifa ya KISIASA na Imetolewa na wanasiasa wa vyama viwili tofauti, japo Mmoja ni Rais wa TLS, hapa utaona sasa Hatari ya kuwa na Rais wa TLS ambae ni mwanasiasa.

2. Taarifa ni BATILI kwa kuwa imeanza kwanza kwa KUHUKUMU kuwa Ofisi za IMMA advocate zimepigwa BOMU na POLISI, japo hizi ni taarifa za AWALI lakini kwa maoni yangu TAARIFA haikupaswa kujielekeza kwenye kazi za mamlaka nyingine, mana kama mmeshajua waliolipua ni POLISI basi hamkuitaji kutoa taarifa Bali kufuata SHERIA kuwashtaki POLISI.

Katika hoja hii MWENDELEZO wake inasema wanavitaka vyombo husika wakiwemo “WATUHUMIWA” Polisi kufanya uchunguzi, mbele zaidi tena wanataka kukutana na “MTUHUMIWA” boss wao IGP, hivi hii ni SAWA WANASHERIA, mnataka kukutana kufanya nini tena na IGP au mkurugenzi wa usalama wa taifa ambae majuzi juzi hapa wakati wa Sakata la Bombadier Rais “WENU “alishema kuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa” ANAMFUATILIA FUATILIA “sasa iweje Leo aombe mwenyewe kukutana na” MTESI ” wake, NDIO MANA NASEMA HAPA KUNA TATIZO YA HIKI CHAMA KUONGOZWA NA MWANASIASA, labda niwakumbushe tu hawa wanasiasa enzi ya Lowassa Walisema” mwizi” alipokwenda kwao wakamuita mfalme wa AMANI hawa ndio wana SIASA.

3. Taarifa ni BATILI, kwa sababu taarifa inataka WANASHERIA kugoma jumanne na jumatano, huu ni MGOMO ambao katika taarifa yao wanaomba ufanywe UCHUNGUZI, lakini pia kwenye taarifa yao wanaomba kuonana na kaimu Jaji Mkuu ambae mmekuja kusema tena hapo Chini ASUSIWE hamtaki kwenda kwenye mahakama anazoziongoza, JAMANI mnajua mnachofanya?

Hii ni sawa na KUJITEKENYA MWENYEWE KISHA UKACHEKA MWENYEWE. nadhani Wasomi wana Sheria tukubaliane katika jambo moja MGOMO au KUONANA na “WATESI “wenu huwezi kushika mambo mawili kwa wakati Mmoja lazima MOJA litaponyoka.

4. Hii taarifa ni BATILI, kwa sababu imemtangaza MGOMO pasipo kusema ADUI ni Nani, hivi Hebu tuambieni mnagoma mkilenga KUMUUMIZA Nani? Kuwaumiza wateja wenu walioko MAGEREZANI au?

Hivi nyinyi hii kazi ya UANASHERIA ni ya kujitolea katika kazi zenu zote? Hivi hakuna pesa mmechukua za wateja wenu ambazo mnapaswa kuzifanyia kazi, au TUSEME na nyinyi “WEZI” mnachukua hela za wateja wenu kisha mnagoma?

Hebu mtuambie Nani ADUI YENU basi.

MASWALI MAGUMU ZAIDI TLS.

1. Hivi Mbona walipouwawa WANASHERIA na MAWAKILI nguli nchini, tena waliowasomesha na kuwafundisha HAMKUGOMA KUSHINIKIZA HAKI ITENDEKE KAMA HIVI LEO, au mmesahau Vifo vya “UTATA” vya Mawakili Marehemu Kapinga, Marehemu Mvungi, Marehemu Mwaikusa? Kwa kuwa mnasahau ngoja tuwakumbushe tu *HAKUNA NAMNA, Leo hao wazee wamekuwa “LIABILITY” kwenu halafu cuf, Lissu, acaccia zimekuwa “ASSET” kwenu?

2. Hivi tangu lini mmeanza kushirikiana press releases na vyama vya siasa mfano cuf?

3. Hivi TLS kimekuwa Chama cha Siasa, au kwakuwa Rais wenu ni mwanasiasa?

4. Mnawezaje kuitenganisha TLS na siasa?

5. Katika Sheria kuna neno linaitwa “INNUENDO” hivi mnajua maana ya hilo neno katika Sakata hili la IMMA advocate?

6. Hivi mnajua IMMA advocate ni kampuni “inayotajwa”  KUCHOTA mabilioni ya fedha za EPA kupitia kampuni ya DEEP GREEN kiasi cha BIlioni 8 zilichotwa, mnajua hilo? kama hamjui nendeni Brella kisha mkasome anuani za Kampuni ya DEEP GREEN, kisha mtangaze MGOMO.

7. Hivi mnajua huyu Rais wenu Lissu akiwa Bungeni mwaka 2012 Aliitaja kampuni ya IMMA advocate kuwa ilizitetea kampuni za TanGold na Deep green microfinances KUCHOTA pesa za EPA, halafu Leo HAWAHAWA imma advocate ndio wanaomtetea Lissu katika kesi zake?

Hivi mnajua maana ya vita ya KIUCHUMI, adui yako anaweza kutumia MKEO, WATOTO* na hata Ndugu zako ili mradi APATE USHINDI.

Mwisho, Nawapenda sana WANASHERIA, mana najua mchango wao katika taifa la Tanzania, nawathamini sana Wanasheria wamaotanguliza UZALENDO kwa taifa Lao pamoja na changamoto tunazopitia kama taifa Changa, Nawapenda Wanasheria wanaosem KWELI kwa maslahi ya taifa Lao na Sio MATUMBO yao.

Sasa Sikilizeni, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.
LEO TUNDU, TUNDUNI.
Wasalamu
Jerry C. Muro
28/08 /2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top