Loading...
Maelfu wamuaga Kigogo UVCCM
*25/08/2017 Mkoa wa Dar Es Salaam*
Viongozi, wananchi, wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka (MNEC) leo wameshiriki katika kuaga mwili wa Marehemu Colman Vincent Masawe Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa 2012-2017
Ibada ya kuaga imefanyika nyumbani kwao Masaki ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Naibu Waziri (OWM) kazi ajira Antony Mavunde, baadhi ya wakuu wa wilaya, Mkuu wa mkoa wa DSM, Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa Neemka, Naibu Katibu Mkuu wizara ya Katiba na sheria Among Mpanju, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mwenyekiti wa UVCCM, wenyeviti wa wilaya, wajumbe wa baraza kuu Taifa, mkoa na wilaya, wabunge wa viti maalum vijana, wabunge wa majimbo ya Mbinga Chalinze na Nzenga, urambo na viongozi wengine mbali mbali wa Chama na Serikali.
Akitoa salam za jumuiya na Chama Cha Mapinduzi Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alisema watamkumbuka marehemu kuwa ni kijana upole, jasiri, mcheshi, mwenye kupenda umoja, upendo kwa wenziwe, lakini kwa uwajibikaji uliongozwa na maadili na nidhamu .
*" Kazi ya Mwenyezi Mungu haina Makosa Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Abdukrahman Kinana kinatoa mkono wa pole kwa wafiwa wote tunawaombea mzidi kuwa na moyo wa ustahamilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba sote tumeguswa na msiba huu tuzidi kumuobea Marehemu Colman mwenyezimungu ampokee kwa amani na ailaze roho ya mpendwa wetu mahali pema, Mbele yetu nyuma yake"*
Marehemu Colman Vincent Masawe amefariki kwa ajali ya gari usiku wa kuamkia jumatano wiki hii msiba umesafirishwa kuelekea kijijini kwao Kibosho Mkoa wa Kilimanjaro kesho jumamosi 26/08/2017.
*Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.*
Post a Comment