Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC Makalla apiga marufuku safari za Wakurugenzi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewapiga marufuku wakurugenzi wa halmashauri, kutoka nje ya mkoa hadi watakapowasilisha ofisini kwake taarifa za maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.

Makalla ametoa agizo hilo, wakati wa  kikao maalum cha baraza la Madiwani katika halmashauri ya Wilaya ya Kyela cha kujadili hoja za utekelezaji wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2015/16.

Makalla amekiri kupokea barua za ruhusa kutoka kwa baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri za kutaka kwenda kwenye ziara mkoani  Dodoma na kwamba amewazuia mpaka watakapowasilisha taarifa za utekelezaji wa sera ya viwanda katika maneo yao.

“Leo ninapambana na Wakurugenzi nimewanyima ruhusa, nimewaambia hakuna kutoka nje ya mkoa huu mpaka waniwasilishie taarifa za maeneo waliyotenga ya viwanda, mmechagua viwanda gani katika halmashauri yenu, maeneo hayo yapo wapi, yamepimwa au hayajapimwa, ripoti hiyo bado sijaipata,” alisema Mhe. Makalla

“Kwa hiyo nyinyi ambao nimeona barua zenu za kuomba ruhusa kwenda Dodoma hakuna kwenda mpaka nipate ripoti hiyo,” aliongeza
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top