Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SERIKALI YAAGIZA FEDHA ZA LGDG ZITUMIKE KWA AJILI YA MAENDELEO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akitoa maagizo kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa fedha za Maendeleo za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGDG) zilizotengwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 249 kwa nchi nzima zitumike kwa ajili ya maendeleo ikiwa ni pamoja na asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka hizo. Wilaya ya Mpwapwa pekee imetengewa milioni 1300.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akitoa maagizo kwa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa fedha za Maendeleo za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGDG) zilizotengwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 249 kwa nchi nzima zitumike kwa ajili ya maendeleo ikiwa ni pamoja na asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka hizo. Wilaya ya Mpwapwa pekee imetengewa milioni 1300.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akikagua jengo la bweni katika shule ya sekondari Kibakwe wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake mwishoni mwa juma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akiangalia ubunifu wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Ipera, kata ya Ipera, kijiji cha Kinusi, wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake mwishoni mwa juma.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akipatiwa maelezo na mwalimu Nsajigwa Mkuu wa shule ya sekondari Kibakwe hatua ambayo maabara imefikia katika ufungaji wa mifumo ya taa na mifereji ya chini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya vitendo kwa masomo ya sayansi wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Lutarawe, kijiji cha Lutarawe, kata ya Ipera wilayani Mpwapwa wakati wa ziara yake mwishoni mwa juma.

............................................................................

Na Fred J. Kibano

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe George B. Simbachawene (Mb) ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutumia fedha za Maendeleo za Mamlaka ya Serikali za Mitaa (LGDG) zilizotengwa katika mwaka wa fedha 2017/2018 kiasi cha shilingi bilioni 249 kwa nchi nzima zitumike kwa ajili ya maendeleo ikiwa ni pamoja na asilimia 10 iliyotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo watumishi wa Mamlaka hizo.

Akiongea katika ziara yake aliyoifanya mwishoni mwa juma, Mhe. Simbachawene amesema kwa sasa hatuna budi kuangalia maendeleo ya Taifa kwanza na sio kuendelea kulipia mambo yasio ya lazima ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za kujengewa uwezo hali ambayo si sahihi kwa maslai ya Taifa na Serikali ya awamu ya tano.

“Halmashauri zote nchini, zitumie hii fedha ya LGDG (Fedha za Maendeleo za Mamlaka za Serikali za Mitaa), fedha ile ya maendeleo kwa ajili ya maendeleo na si vinginevyo, na maendeleo ninayoagiza kwa Halmashauri zote nchini yawe yanalenga kumaliza maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi kama miradi iliyopita”

Ameyataja mfano wa baadhi ya maboma ambayo yanastahili kutumia fedha hizo yaliyopo wilayani Mpwapwa ni kama madarasa ya shule ya msingi Wangama, Maabara ya Mbuga sekondari, shule ya msingi Shikizi na mengineyo ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi.

Mchanganuo wa fedha hizo ambao ni shilingi bilioni 249 asilimia 80 ni kwa ajili ya shughuli za maendeleo, asilimia 10 kwa ajili ya kazi za usimamiaji na asilimia 10 kwa ajili ya kujengewa uwezo ambazo zimekatwa na kuwekwa kwa ajili ya maendeleo.

“Lakini asilimia 10 ambayo inasema ni kujengewa uwezo, ambayo ni watu wanakwenda semina, warsha, mara waite ‘workshop’, hii hapana, hii fedha yote iende kwa ajili ya miradi ya wananchi hasa kwenye maboma. Tunayo maboma mengi sana, hasa sekta ya afya, elimu na mengineyo”

Mhe. Waziri Simbachawene amesisitiza kuwa hata wakati akihitimisha hotuba yake katika bunge la bajeti alitoa kauli ya matumizi ya fedha hizo. “ Nilipokuwa nafunga hotuba yangu kwenye bunge la bajeti nilielekeza asilimia 60 tuipeleke kwenye miradi ya afya na kwa hivyo narudia hapa kusema asilimia inayobaki yote iedne kwenye miradi ya elimu, kasoro ile asilimia 10 usimamiaji kwa sababu ni lazima miradi ili iwe mizuri, lazima isimamiwe” , alisema.

Aidha, amesema Serikali itatoa waraka maalum kuonyesha mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo maalum za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ndani ya mwaka huu wa fedha  wa Serikali.


Mheshimiwa Simbachawene anafanya ziara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hasa maeneo ya vijijini ili kujionea hali halisi ya utendaji, migogoro ya ardhi, utunzaji wa mazingira, huduma kwa wananchi na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ambapo mwishoni mwa wiki ametembelea kata za Mbuga, Kibakwe na Ipera zenye vijiji kadhaa wilayani Mpwapwa kama sehemu ya kazi zake za kujionea maendeleo ya wananchi na kero zao.  
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top