Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa kutoka uwanja wa Taifa kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja huo sehemu ya pitch imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo Alex Nkenyenge amevunja ukimya na kufunguka yafuatayo;
“Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa limeshaliwa
“Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyoletwa ambao tulikuwa tunajaza kwenye pitch baada ya kuwa tumeondoa lea ya juu
“Kwa hiyo hakuna kitu kama hicho bahati mbaya kwa watanzania wanapenda kuzungumza vitu vibaya kuliko vizuri, maana mtu haulizi wala kushangaa ile inayosafisha uwanja, sasa kama ni fuvu unataka kusema uwanja wa Taifa kulikuwa na makaburi?”
Post a Comment