Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM kuendelea kutetea na kusimamia fursa kwa Wanawake

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshiriki katika Tamasha la Kijinsia linaloandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) jijini Dar Es Salaam.
Katika siku yake ya mwisho ya Tamasha hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ametembelea maonesho ya kazi mbalimbali za wajasiriamali wanawake na taasisi mbalimbali za kiraia na akapata nafasi ya kuwa sehemu ya shughuli ya kuahirisha Tamasha ambapo maazimio ya kuimarisha haki na nafasi ya wanawake na ujinsia yalisomwa.
Ndg. Polepole amewahakikishia wanawake wa Tanzania kupitia washiriki wa Tamasha kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaendelea kuweka kipaumbele agenda ya ujinsia na maendeleo na kuielekeza serikali kusimamia ipasavyo kuachiliwa fursa zaidi na hasa za kifedha kwa wanawake kupitia mifuko mbalimbali ya fursa za kifedha na asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kuwezesha wanawake na vijana.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top