Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM yaanika walichojadili .... Yafafanua alipo Kinana na Wabunge wanaosadikiwa kuvuliwa vyeo



ALIYOYASEMA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI TAIFA NDG. HUMPHREY POLEPOLE OFISI NDOGO YA CCM, LUMUMBA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 30, 2017

"Chama cha mapinduzi kimefanya uchaguzi wake mpaka sasa kwa mafanikio makubwa sana.Mashina ya chama yameimarika" - Polepole

"Kwa nchi nzima ccm ina mashina zaidi ya laki mbili na ishirini na mbili na Chaguzi zimekamilika zaidi ya 97%"- Polepole

"Nec imeridhia kuelekeza wilaya zifuatazo nafasi za uwenyekiti zitatangangazwa upya
Moshi mjini,siha,Hai,Makete" - Polepole

"chama kimejiridhisha kwamba wagombea waliojitokeza walikuwa na kasoro za kimaadili na kikanuni Na walikuwa na  viashiria hatarishi kwa chama" - Polepole

"Wako ambao wameanza kampeni kuelekea chaguzi zinazofuata za dola kule Zanzibar kikao NEC imewataka kuacha mara moja"-Polepole

"Ni mwiko kutoa rushwa ama kupokea.Kufanya kampeni kabla ya wakati ni marufuku"-PolePole

"Wale ambao hawataona kama kuna haki imetendeka watoe malalamiko ndani ya wiki mbili"-Pole Pole

"Kanuni ya uchaguzi wa ccm fungu 28 inazungumzia malalamiko ya uchaguzi,kabla,wakati ama baada ya uchaguzi kufanyika"-Polepole

"Wale ambao watapewa dhamana kwenye ngazi ya wilaya watapaswa kuachia nafasi za chini, Rushwa haitavumiliwa Kwenye uchaguzi wa CCM"-PolePole

"Chama kinanisisiza Mtu mmoja kuwa na cheo kimoja.Mtu mmoja Kofia moja"-Polepole

"Nidhamu ya chama Kwenye uchaguzi, Chama kitafuta chaguzi zitakazokuwa zimekiuka miiko na kanuni za uchaguzi"-PolePole

"NEC inaendelea kukumbusha wale wote walioteuliwa kushiriki chaguzi  wanapaswa kuzingatia kanuni za maadili na kanuni za uchaguzi"- Polepole

"wilaya ya Musoma kuundwa kwa wilaya za kichama mbili ambazo ni
Wilaya ya kichama ya msoma mjini na wilaya ya kichama ya musoma vijijini."- Polepole

"Vyama vya upinzani wako mstari wa mbele kujua hali ya viongozi wa Ccm,hii inatufurahisha sana sisi CCM"-Polepole

"Kinana anauguliwa na mwanafamilia wake wa karibu.Anauguza mgonjwa"-PolePole

"Kinana amekuwepo Kwenye maandalizi ya vikao hivi mpaka hatua za mwisho" - Polepole

"Hakuna barua ya Kinana kujiuzulu,Naomba wana ccm na watanzania wapuuze gazeti la Tanzania Daima kwa upotoshaji"-Polepole

"Hatujawakata wagombea kwa sababu za kuwa mahusiano na Lowassa"-Polepole

"Hakuna taarifa za kuwafukuza wabunge wa ccm .Ni uzushi wa vyama vya upinzani vilivyokosa ajenda"-PolePole

"Hakuna Kosa ama uvunjifu wa sheria kwa Ccm kufanyia vikao vyake ikulu"-Polepole

Imeandaliwa na:

Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Credit: DarMpya
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top