Wanafunzi 917,072 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi kesho na keshokutwa (Septemba 6 na 7).
Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 432,744 sawa na asilimia 47.19, wakati wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81.
Watahiniwa 882,249 watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na 34,823 watatumia lugha ya Kiingereza.
Jumla ya watahiniwa 94 wasioona wamesajiliwa kufanya mtihani huo, wakiwemo wavulana 58 na wasichana 36.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema maandalizi yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa vifaa vinavyohitajika katika halmashauri zote nchini.
Dk Msonde amezitaka halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani unazingatiwa.
"Tunataka mazingira ya vituo vya mitihani yawe salama, tulivu na kuzuia mianya yoyote inayoweza kusababisha udanganyifu,” amesema.
Post a Comment