Aliyekuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Hashim Rungwe anashikiliwa na polisi kwa siku nne sasa.
Rungwe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Chaumma anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mwanasiasa huyo anashikiliwa akituhumiwa kughushi nyaraka.
Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema jana Septemba 5 kuwa, Rungwe anashikiliwa kituoni hapo kwa siku nne.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo akisema hana taarifa za kutosha.
Post a Comment