Na Mwandishi wetu,
Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM)
umesema kimsingi utaratibu wa kushughulikia mambo mbali mbali ndani ya Chama na
Jumuiya zake uko wazi na Mtu mwenye madai au tuhuma hutakiwa kutumia
vikao halali vya kikanuni na kikatiba .
Pia umoja huo umesema
kwa mwenye dukuduku na hoja za msingi huzifikisha kwa viongozi ili
hatua na utaratibu huweze kufuatwa.
Msimamo huo umetolewa na
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndg.Shaka Hamdu Shaka alipozungumza na waandishi wa
habari Makao Makuu ya UVCCM Upanga jijini Dar es salaam.
Shaka alisema
kila mwana jumuiya muadilifu, msemakweli, mpenda Umoja na Mshikamano,
siku zote huheshimu kanuni, taratibu, katiba na maelekezo yanayotolewa na
viongozi bila kuleta mgawanyiko .
Alisema huku akiwaasa
na kuwaonya wale wote ambao pengine watakuwa wameteleza na kujikuta
wakijielekeza na kushiriki vitendo ambavyo ni kinyume na taratibu halali.
"Wapo tunaowajua
wakishiriki vitendo hivyo na kadri itakavyothibitika kwa kukusanya
ushahidi na vielelezo, hatua za kikanuni, kikatiba na pale itakapobidi
hatutasita kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria ili liwe funzo kwa
wengine"Alisema.
Alisema Umoja huo usingalipenda
kuona watu wakijitwika na kubeba agenda binafsi huku wengine wakidhania
kumchafua mtu ndio wepesi wa kupata cheo ndani ya chama au Jumuiya.
"Mtu yeyote
atakayeendelea kufanya hivyo kwa kisingizio cha uchaguzi wa Chama na Jumuiya
zake, tutamkabiri kwani mambo haya hayakubaliki”.Akisisitiza
Kaimu huyo Katibu Mkuu
pia alizungumzia mwenendo na mchakato wa Uchaguzi ndani ya jumuiya hiyo ikiwemo
na kutaja idadi ya wagombea waliojitokeza katika nafasi mbalinbali.
Alisema uchaguzi ni
kipimo cha upevu na kielelezo cha ukomavu wa demokrasia bila mizengwe ndani ya
chama na Jumuiya zake kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi
itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu .
"Dhana ya
Demokrasia ni muhimu kuheshimiwa na ndani ya Chama na Jumuiya zake.
Kiongozi wa UVCCM mahali popote pale huchaguliwa kwa kufanyika uchaguzi huru nawa
haki unaozingatia Kanuni na taratibu za Uchaguzi bila ya kukiuka,
au kuvunjwa"Alieleza.
Shaka alisema nia ya
UVCCM ni kujenga na kudumisha haiba njema ya kuheshimu misingi ya Demokrasia
yenye kuchunga adabu , nidhamu, miiko na maadili kwa kila mwanachama
anayetaka kuchagua au kuchaguliwa.
Akizungumzia Uchaguzi
ndani ya jumuiya hiyo alitaja Uchaguzi wa UCCM ulianza ngazi ya Matawi
ambapo hadi sasa jumla ya Matawi 23, 529 sawa na Asilimia 99.4 kati ya Matawi
23, 529 sawa na Asilimia 0.59 yamekamilisha uchaguzi.
Katika ngazi za
Kata 3, 913 sawa na Asilimia 96.59 kati ya kata 4,051 sawa na asilimia
3.4 zimekamilisha uchaguzi .Kwa upande wa majimbo ya Zanzibar majimbo 54
sawa na Asilimia 100 .
Pia uchaguzi,
ngazi ya Wilaya na Mkoa matauarisho yake yanaendelea vizuri huku mchakato
wa uchujaji majina kwa waombaji nafasi mbali mbali ndani ya unaendelea vizuri
ambapo jumla ya Vijana 7,606 wamechuka fomu.
Kwa upande wa ngazi ya
Taifa Vijana 382 wamejitokeza kuomba nafasi za uongozi na kati yao 114 nafasi
ya Mwenyekiti wa Taifa, 22 Makamu Mwenyekiti, 144 Halmashauri Kuu ya Taifa, 15
nafasi ya uwakilishi kutoka Vijana kwenda Wazazi na 14 nafasi ya
uwakilishi kutoka UVCCM kuenda UWT.
Alisems maandalizi kwa
ajili ya mikutano Mikuu ya Wilaya hadi Taifa yanaendelea vyema ambapo chaguzi
zote ndani ya UVCCM zinategemewa kukamilika Novemba mwaka huu.
"Tusisitiza kuwa
sifa na wasifu wa kila mgombea kwa kadri alivyojaza kwenye fomu yake,
utaandikwa vizuri katika kitabu maalum cha wagombea wote ambacho watapatiwa
wajumbe wa Mkutano siku ya uchaguzi"Alisema.
Aidha mgombea atapata
nafasi ya kujieleza na kutoa wasifu wake, kutaja dhamira na malengo yake mbele
ya wajumbe wa Mkutano Mkuu husika si kinyume na hivyo baada ya taratibu
za vikao kukamilika.
Kaimu huyo Katibu Mkuu
alisema wanawakumbusha kuwa ni mwiko kwa mgombea kuanza kampeni mapema au
wapambe wake kufanya ushabiki wa kisiasa kumnadi, kumpigia debe au kujipitisha
ukiukaji huo utampotezea mgombea sifa za kuteuliwa .
"Kuyaacha hayoyafanyike
bila ya kuyadhibiti, kuyaasa na kuyakemea ni njia ya kukaribisha mvurugano,
mgawanyiko hatimaye kujipenyeza kwa adui rushwa. Hivyo basi
tunawaagiza watendaji wote wa ngazi husika kusimamia matakwa ya kikanuni,
kimaadili na kikatiba.
Shaka ameviomba viomba
vyombo vinavyohusika hasa TAKUKURU kufuatilia nyendo za wagombea na wapiga kura
ili kubaini endapo wako watakao kwenda kinyume na sheria.
Alisema Mgombea au mpiga kura yoyote
atakaethibitika kutoa au kupokea rushwa, hatua za kimaadili na kisheria tunaelekeza
zichukuliwe ili kulinda heshima ya Chama na Jumuiya.
Post a Comment