Na. Paschal Dotto-MAELEZO
Katika kuelekea ujenzi wa Tanzania ya uchumi wa kati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli, Kiongozi anayesifika kwa uchapakazi, mtu wa watu, mtu wa wanyonge na Mzalendo kwa kusimamia rasilimali za Taifa ambaye ameonyesha nuru kubwa kwa watanzania.
Katika hotuba zake mbalimbali amekuwa akisisitiza wananchi kufanya kazi na kuienzi kauli mbiu yake “HAPAKAZI TU” huku katika utendaji kazi wake Rais Magufuli ameonesha dira kubwa kwa kuanza na miradi mikubwa ambayo itaipeleka nchi katika uchumi wa kati na wenye viwanda na huduma nzuri kwa jamii, watanzania wanatakiwa kumuunga mkono ili aweze kuifanya kazi yake kwa ufasa kwa kuanzisha, kuendeleza na kumalizia miradi ambayo ipo mikononi mwake.
Kama alivyoahidi wakati wa kampeni kwamba Serikali yake itakuwa ya kuchapa kazi huku akiwa mstari wa mbele katika kuchapa kazi na alipewa jina la uchapakazi kama Tinga Tinga yani mtu wa kazi, ni miradi mingi ambayo Serikali yake imefanya na inaendelea kufanya mambo makubwa Kama yalivyoainishwa na mwandishi wa makala hii.
1. Barabara za Juu (Fly Over).
Aprili 16 ya mwaka 2016 uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara za juu ulifanyika Jijini Dar es Salaam katika makutano ya barabara ya Tazara ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, barabara ambayo itaondoa msongamano wa magari katika Jiji hilo na kuweza kusaidia kuokoa upotevu wa mapato utokanaona watu kuchelewa kazini na kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Faida kubwa ya barabara hii itatupunguzia fedha zilizokuwa zikipotea, katika tafiti zilizofanywa mwaka 2013 tulipoteza billion 411.3 katika Jiji la Dar es Salaam pekee kwa sababu ya msongamano mkubwa”, alisema Rais Magufuli.
Mradi huu mkubwa ambao utagharimu fedha za kitanzania shilingi billion 101.6 unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Japan (JAICA), ambapo Shirika hilo litatoa kiasi cha shilingi billion 93.44 na Tanzania ikitoa billion 8.36,Mradi huu ambao ni wa aina yake Tanzania unatarajia kumalizika ifikapo oktoba 2018, huku barabara nyingine ya aina hiyo iliyoko makutano ya Ubungo ikitarajiwa kamilika ifikapo 2020 na kuwezesha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kufurahia maisha kwani sasa wataondokana na adha ya usafiri hivyo kuwahi kwenye maeneo yao ya kazi kuchapa kazi na kuijenga Tanzania ya viwanda.
2. Bomba la Mafuta Ghafi (Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanzania).
Ilikuwa ni siku ya pekee kwa wananchi wa chongoleani ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseveni walizindua mradi mkubwa ambao ni wa kipekee duniani.
Ni bomba ambalo lina urefu wa kilomita 1445 huku Tanzania likichukua sehemu kubwa yaani kilomita 1115 na kilomita 130 ni kwa upande wa Uganda, ni mradi ambao utagharimu kiasi cha dola za Kimarekani billion 3.5 na utasimamiwa na kampuni tatu yaani SNOOC,TOTALE zote kutoka nchini Ufaransa pamoja na TUROL ya Uingereza na unatarijia kukamilika mwaka 2020.
“Ni mradi wa kipekee duniani kwa kuwa mradi kama huu upo India ambao unasafirisha mafuta ghafi lakini una kilomita 600 tu, kwa hiyo bomba hili ni la kwanza duniani”, alisema Rais Magufuli.
Mradi huu utapita katika Mikoa nane kwa Tanzania bara Wilaya 24 huku Vijiji 184 vikifaidika na mradi huo mkubwa wa kipekee ambao utatoa ajira 10,000 wakati wa ujenzi na 1,000 kwa uendeshaji wake, Wahenga walisema “Kizuri kula na nduguyo” ndivyo ilivyo kwa Rais Museveni wa Uganda kukubali kushirikiana katika mradi huu mkubwa kwa kupata ushawishi mkubwa wa usalama kutoka kwa Rais mchapakazi Dkt.John Pombe Magufuli (Tinga Tinga).
3. Kufufua Shirika la Ndege (Air Tanzania).
Serikali ya Awamu ya Tano ilianzisha nia na matumaini katika kukuza na kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa kufufua shirika lake la ndege (ATCL) ambalo mwaka 2016 lilianza rasmi baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kununua ndege zake mpya ambazo zimekuwa zikisaidia Watanzania hususani wafanya biashara waendao mikoani mara kwa mara kwa kupunguza gharama kubwa za usafiri.
“Tumeleta bombardier Q 400 imepunguza gharama za safari kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza wanalipa 160,000 hadi 200,000 wakati nauli ilikuwa imeshafikia hadi 800,000 kwa safari za Dar es Salaam –Mwanza”, alisema Rais Magufuli.
Mnamo septemba 2016 serikali ya awamu ya tano ilileta ndege mbili aina ya Bombadier Q400 ambazo litengenezwa nchini Canada, katika matarajio yake inatarajia kuwa na ndege 7 ambapo kwa awamu ya kwanza zimekuja mbili , lakini pia ndege mbili aina ya Jeti CS 300 zenye uwezo wa kubeba abiria 137-150 zitaletwa nchini 2018 , bila kusahau ndege kubwa aina ya Boen 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ambayo nayo italetwa waka 2018, itasaidia kwa safari za kimataifa kwani itakuwa na uwezo wa kutoka moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere hadi Marekani ama Ulaya bila kutua kokote.Huu ni mradi ambao utaleta fursa ya maendeleo hususani katika sekta ya utalii.
4. Sekta ya Utalii.
Sekta ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameendelea kuinua zaidi ni Sekta ya Utalii baada ya ununuzi wa ndege ambazo zitakuwa kimbilio katika kukuza na kuimarisha Utalii nchini.
“Huwezi kuendeleza nchi bila kuwa na Watalii sisi tunazungumza Watalii hawajaweza kufika hata milioni 2, lakini nchi kama Morocco inapokea Watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka kwa hiyo ni vyema kushirikana nao katika masuala ya Sekta ya Utalii”, alisema Rais Magufuli.
Sekta ya Utalii ni chachu kwa maendeleo ya Taifa kwani inalipatia pato kubwa na kuweza kuimarika kiuchumi kupitia fedha za kigeni, lakini kwa Tanzania kumekuwa na upungufu wa ndege kwa kuliona hilo Serikali ya Awamu ya Tano imeweza kununua ndege kubwa aina ya Boen 787-8 dreamliner ambayo itakuwa inatoka moja kwa moja kutoka Ulaya, Amerika na kwingineko duniani na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
“Tunataka Watalii wawe wanatoka Marekani wanakuja moja kwa moja Dar es Salaam, ile ndege inauwezo wa kutoka Marekani, Australia bila kutua popote”, alisema Rais Magufuli.
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendeleza Utalii kwa kuingia makubaliano na nchi mbalimbali ikiwemo Serikali Morocco kupitia ziara ya Mfalme Mohammed VI ,ya mwaka 2015 ambapo waliingia makubaliano ya mkataba kwa Sekta ya Utalii unaolenga kubadilishana Watalii kwani nchi ya Morocco ina idadi kubwa iliyofikia milioni 12 kwa mwaka 2015 na idadi hiyo inatarajia kuongezeka mpaka milioni 14 mwaka 2017 kwa hiyo ni vyema kuwa na ushirikaiano ili kukuza Sekta hii nchini.
5. Mradi mkubwa wa umeme (Kinyerezi I na II).
Juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano yenye malengo makubwa katika kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda imetambua kuwepo kwa viwanda kunaambatana na nishati ya uhakika ya umeme kwa hiyo Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameweza kuanzisha mradi mkubwa wa umeme ili kuendana na Sera yake ya Tanzania ya viwanda.
“Umeme ni maendeleo, umeme ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi kwa Taifa lolote duniani, bila ya kuwepo kwa umeme wa uhakika ndoto yetu ya kujenga uchumi wa viwanda haitaweza kutimia”, Rais Magufuli.
Katika mradi huu wa umeme ulianza na kinyerezi I ambayo itaweza kutoa megawati 150 lakini katika uzinduzi wa ujenzi wa kinyerezi II ambayo itatoa megawati 240 kwa watanzania, Mradi huu wa kinyerezi II ambao unafadhliwa na Serikali ya Japan iliyotoa dola za kimarekani milioni 292 ambayo ni asilimia 85 ya ujenzi huku Tanzania ikitoa dola milioni 120 ambayo ni sawa na asilimia 15 ya mradi, Uzinduzi huu uliambatana na ongezeko la megawati kinyerezi I ambapo megawati 180 zitakazogharimu dola milioni 20 jumla ya megawati 330 zitapatikana katika Mradi huo na hii ni faida kubwa kwa Watanzania wote kwani wataweza kuanzisha viwanda vidovidogo na hatimaye kukuza uchumi.
“Tunataka tuwe kama nchi zingine duniani kwa matumizi ya umeme sisi bado tuko wati 30 kwa kila mtuamiaji wa nishati hii, lakini Kenya wati 40, China wati 490, Afrika ya Kusini wati 500 na Marekani wati 1,683 kwa kila mtu kwa hiyo sisi bado tuko nyuma”, Rais Magufuli
Katika mradi huu ambao utajengwa kwa awamu yaani kinyerezi I mpaka VI utasaidia kuondokana na adha ya umeme nchni.
Kwa uchache hayo ndio baadhi ya mafanikio ambayo JPM ameweza kuyafikia katika kipindi kifupi alichokaa madarakani, hii ni ishara kuwa hadi atakapomaliza muhula wake Tanzania itakuwa imepaa kiuchumi na kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali.
Post a Comment