Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mbunge Peter Msigwa akamatwa na polisi Mkoani Iringa

Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa (Chadema) amekamatwa na polisi Jana Jumapili jioni baada ya kushushwa jukwaani kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege mkoani Iringa.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema Iringa Mjini (Bavicha), Leonce Marto amesema  kuwa mbunge huyo alikamatwa saa 11:24 jioni na Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) aliyekuwa ameambatana na polisi wengine kisha wakampeleka ofisi za mkoa za jeshi hilo.

“Kutoka Mlandege mpaka ofisini kwa kamanda wa mkoa amebadilishwa kwenye magari matatu. Tunahisi atakuwa anasafirishwa ingawa bado anahojiwa. Yupo ndani, sisi tunaendelea kumsubiri nje,” amesema Marto.

Mwenyekiti huyo alibainiha  kwamba mpaka wakati huo (saa 12:30 jioni) jeshi hilo halikubainisha sababu za kumshikilia Msigwa.

“Alikuwa na kibali cha kufanya mkutano katika kata tatu kuanzia leo Jumapili mpaka Jumanne. Alianza kuzungumza saa tisa alasiri ilipofika saa 11:24 jioni, RCO akiwa na polisi wengi wakamshusha jukwaani na kuondoka naye,” alisema Marto bila kufafanua sababu za kukamatwa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top