Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Rais Magufuli asali kanisa la Wasabato .... Amwaga neema


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti pamoja na  mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakiombewa sala  na Maaskofu wa Kanisa hilo la Waadventista Wasabato, Sala iliyokuwa ikiongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Marc Walwa Malekana(wa kwanza kushoto)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakikabidhi mifuko 400 ya Saruji itakayotumika katika ujenzi wa Kanisa hilo la Wasabato la Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mama Navana Cable aliyeambatana na mtoto  wake Rebecca Cable ambao familia yao imeahidi kumalizia ujenzi wa Kanisa hilo la Waadventista la Wasabato mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuendesha Harambee ya Papo kwa papo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mhariri Mtendaji waMagazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jim Yonaz mara baada ya kuahidi kuchangia katika kanisa hilo.
 Waziri Mstaafu katika awamu iliyopita Steven Wasira naye akichangia katika Harambee hiyo Kanisani hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Ndugu Dkt. Edward Hosea mara baada ya kuchangia katika ujenzi wa kanisa hilo la Wasabato lililopo Magomeni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshika mkono mtoto ambaye alikua anamsalimia wakati akitoka ibadani katika kanisa hilo la Magomeni.
Waumini mbalimbali wa Kanisa hilo wakiwa ibadani kama wanavyoonekana pichani. PICHA NA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amepiga magoti na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Waumini wengine wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai katika Ibada ya Jumamosi kanisani hapo  jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakiimba nyimbo katika ibada hiyo ya Jumamosi katika Kanisa la Waadventista Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na   mkewe Mama Janeth Magufuli wakisikiliza neno katika Ibada hiyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisoma neno pamoja na mkewe Mama Janeth Magufuli kanisani hapo wakati wa Ibada ya jumamosi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa la Waadventista la Wasabato Ushirika wa Magomeni Mwembechai  kabla ya kuendesha Harambee ya Ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya Sh. 25milioni ziliahidiwa kukusanywa.
****
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli leo tarehe 02 Septemba, 2017 wameungana na waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Usharika wa Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam kusali Ibada ya Sabato.

Ibada hiyo imeongozwa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania, Baba Askofu Mark Walwa Malekana aliyekuwa pamoja na Askofu wa Jimbo la Mashariki Kati, Baba Askofu Joseph Mgwabi na Askofu wa Jimbo la Kusini Mashariki, Baba Askofu Albert Nziku.

Akizungumza baada ya Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amelipongeza Kanisa hilo kwa kutoa huduma ya kiroho kwa waumini wake na pia kutoa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali nchini, na amewahakikishia waumini na viongozi wake kuwa Serikali inatambua mchango huo na itaendelea kushirikiana na madhehebu yote ya dini katika kuwahudumia wananchi.

“Baba Askofu nakushukuru sana kwa mahubiri mazuri ya leo ambayo yamenigusa sana, madhehebu ya dini likiwemo hili la Waadventista Wasabato mnatoa mchango mkubwa sana kwa Taifa letu, nakuhakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nanyi” Amesema Mhe. Rais Magufuli.

Pamoja na kushiriki Ibada hiyo Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa jipya la Waadventista Wasabato Usharika wa Magomeni Mwembechai, amechangia Shilingi Milioni 1 kwa kwaya za Kanisa hilo na pia ameendesha harambee ya papo kwa papo ya kuchangia ujenzi wa Kanisa, na kufanikisha kupata Shilingi Milioni 25.3.

Baba Askofu Mark Walwa Malekana amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya Sabato na kuchangia ujenzi wa kanisa, na ameongoza maombi ya kuliombea Taifa na Rais.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
02 Septemba, 2017
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top