Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa nchi Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kutoa ajira kwa wanajeshi 3000 wapya mwaka huu, ili jeshi la Tanzania liweze kuwa na askari wa kutosha.
Rais Magufuli ametoa taarifa hiyo leo alipokuwa akihutubia umma mara baada ya kuwapa kamisheni maafisa wa Jeshi, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, huku akitaka wahusika kutowasahau vijana waliohitimu mafunzo ya JKT.
"Lakini pia leo tumepata maofisa 422, unapokuwa na jeshi la maofisa lazima kuwepo na 'junior officers', huwezi ukawa na jeshi lote lina maofisa, kwa kutambua hili natangaza rasmi kwamba nitatoa nafasi 3,000 za kuajiri wanajeshi wapya, na hawa wataoajiriwa muzingatie na wale ambao wamemaliza JKT, lengo ni kuhakikisha jeshi letu linakuwa na maaskari wa kutosha na la kisasa zaidi", amesema Rais Magufuli.
Leo Rais Magufuli ametoa kamisheni kwa Maafisa wa Jeshi 422 waliohitimu mafunzo katika chuo cha Monduli, hafla ambayo imekuwa ya kwanza kufanyika katika uwanja wa umma
Post a Comment