Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RC MAKONDA AENDELEZA KASI YA DAR ES SALAAM YA VIWANDA






Katika kuunga mkono DIRA ya Mhe Rais, *Dkt. John Pombe Magufuli* ya Tanzania ya *VIWANDA*, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam _Mhe Paul Makonda_ *AMEZIAGIZA* manisapaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam kubadilisha Mfumo wa *UTOAJI WA asilimia 10%* kwa kina mama na vijana ili fedha hizo ziweze kuleta *TIJA* katika kutekeleza wa *DIRA* ya taifa ya kuwa na Tanzania ya viwanda.

_Mhe Makonda_ amesema mfumo wa sasa hauna *UTAMBUZI* wa kutosha kwa vijana na kimama kutokana na Makundi hayo kutawanyika kibiashara jambo linalosababisha changamoto ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo, na badala yake Kuzitaka Manisapaa kutenga maeneo maalum ya uanzishaji wa *VIWANDA VIDOGO VIDOGO* kwa ajili ya makundi hayo, hatua itakayowaweka pamoja na hivyo kutoa fursa kwa serikali ya Mkoa kuwahudumia vizuri.

_Mhe Makonda_ amesema katika kutekeleza Mpango huo Leo ameamua kuzinduzi majengo yatakayotumia kwa ajili ya uanzishaji wa *VIWANDA VIDOGO VIDOGO* katika eneo la Mwananyamala manisapaa ya *KINONDONI* ili kuzihimiza manisapaa nyingine kuiga mfumo huo.

Katika hatua nyingine, Mhe Paul Makonda *AMEWATAKA* wafanyabiasha *NDOGO NDOGO* (Machinga) kuanza kuuza *BIDHAA* zinazozalishwa nchini na viwanda vya wawekezaji walio Tanzania, pamoja na *BIDHAA* zinazozalishwa na wajasiriamali wadogo wadogo ili kuongeza wigo wa kukua kwa uzalishaji wa bidhaa zinazozalishwa Tanzania, amewataka *WAMACHINGA* nao kuonyesha *UZALENDO* kwa vitendo kama anavyofanya Rais Mhe, *Dkt. John Pombe Magufuli* ambae siku zote ameonyesha *MOYO* na *NIA* ya kuwasaidia *WAMACHINGA* nchini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top